Waziri wa Katiba na Sheria, Prof Palamagamba Kabudi akizungumza katika mkutano wake na Mtandao wa Kutetea Mashirika yanayotetea haki za biandamu (THRDC) jijini Dodoma.
Mratibu wa mtandao wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa akizungumza katika mkutano wao na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof Palamagamba Kabudi uliofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof Palamagamba Kabudi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara yake na Maafisa kutoka Mtandao wa THRDC mara baada ya kumaliza mkutano wao wa pamoja.

Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa kutetea Haki za Binadamu ili kuhakikisha wananchi wanapata haki  kama ilivyohainishwa katika katiba na ilani ya chama cha mapindizi (CCM) ya mwaka 2020/2025.

Akizungumza na watumishi wa Mtandao wa Kutetea Mashirika yanayotetea haki za Binadamu (THRDC) Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi amesema Serikali haina budi kushirikiana na wadau wenye nia ya kutetea wananchi na hasa wanyonge.

"Tuko tayari kushirikiana na wadau ninyi muhimu kwenye masuala ya kupigania haki za wananchi tunajua kuwa mtakua na vipaumbele vyenu muhimu na serikali pia itakuwa na vipengele vyake  ambavyo vinalenga kukuza haki za binadamu  nakuleta maendeleo katika nchi yetu,

"Hayo yote ni matakwa ya ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025  kuwa serikali imeahidi kuheshimu na kuzingatia haki za binadamu kwa mtu mmoja mmoja, makundi na makundi ili kujenga jamii yenye usawa," Amesema Waziri Kabudi.

Amesema Tanzania sio nchi ya kufundishwa kupigiania haki za binadamu kwani ni suala ambalo lilianza tangu zamani sana na kila kitu kimeandikwa kwenye katiba.

Kwa Upande wake Mratibu wa Mtandao wa THRDC Onesmo Olengurumwa  amesema serikali inatambua kuwa mfumo bora wa sheria ndio msingi wa kutekeleza matakwa ya katiba, sera na mpango wa nchi.

Amesema asasi za kutetea haki za binadamu zimekuwa na mchango mkubwa kwa jamiii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati.

"Asasi za kiraia zimekuwa zikifanya vizuri sana hapa nchini tunaomba serikali itambue mchango wa asasi hizo na kuongeza ushirikiano ili zziendelee kufanya vizuri kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla," Amesema.

Olengurumwa ameihakikishia serikali kuwa mashirika ya kutetea haki za binadamu yataendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati bila vipingamizi vyovyote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...