Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

SIMBA SC rasmi imeifuata Young Africans katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) msimu huu baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Majimaji mkoani Ruvuma.

Bao pekee la Simba SC lililozua utata limefungwa na Luis Jose Miquissone katika dakika ya 88 baada ya Mchezaji Bernard Morrison kuangushwa nje kidogo ya lango la Wanarambaramba kutoka Chamazi mkoani Dar es Salaam.

Azam FC walionekana kucheza maridadi dakika zote 90 kwa kuimudu Simba SC katika mchezo huo, Janja janja ya Morrison ndio iliyoamua mchezo huo kuisha ndani ya dakika 90 bila kwenda dakika 120 au matuta (Penalti).

Nahodha wa Azam FC, Agrey Moris baada ya mchezo kuisha amesema wamezembea katika nafasi moja hadi kuwagharimu na kushindwa kufuzu Fainali ya Michuano hiyo ambayo Bingwa anawakilisha nchi katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Julai 25, 2021 ni rasmi Simba SC na Yanga SC zitacheza katika mchezo wa Fainali ikiwa ni baada ya kucheza Julai 3, 2021 katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu huu. Yanga SC walifuzu Fainali ya Michuano hiyo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United ya Mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...