Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Sportpesa, Sabrina Msuya (kushoto) akielekezea jinsi bidhaa hiyo ya Nambari za Bahati (Lucky Numbers) inavyochezwa na Wateja.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Sportpesa, Sabrina Msuya akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi zao wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya Nambari za Bahati (Lucky Numbers).


 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa imezindua bidhaa yake mpya ya Lucky Numbers (Namba za Bahati) katika mwezi huu ikiwa na nia ya kutanua wigo la michezo na kuwapa nafasi wateja wake kufurahia mchezo huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika uzinduzi huo, Meneja Uhusiano na Mawasiliano, Sabrina Msuya amesema wamezindua huduma hiyo ikiwa na michezo zaidi ya 160 yenye masoko zaidi ya 14 kwa ajili ya wateja wake kuwa na wigo mpana katika michezo ya kubashiri.

Msuya amesema mteja wa Sportpesa anaweza kucheza Nambari za Bahati akiwa amejisajili na kuweka pesa kwenye akauti yake.

“Unacheza mchezo wa Nambari ya Bahati (Lucky Numbers) kwa kuchagua mchezo uupendao kwa kuzingatia muda uliopagwa kucheza, baada ya kuchagua utapokea masoko zaidi ya 14 yanayopatikana kulingana na droo uliyochagua”, amesema Msuya.

“Weka dau lako kwa kuweka kiasi cha kucheza kisha weka ubashiri wako. Mara baada ya droo kuchezwa matokeo hupatikana kwenye tovuti na APP yetu”, ameeleza.

Huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti ya Pamoja na APP ya Sportpesa kwa Mitandao yote ya Simu kuanzia kima cha chini cha Shilingi 50 za Kitanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...