John Nditi, Morogoro

TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imezindua Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kwenye viwanja vya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere(Nanenane) Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro ambacho kitatumika kutoa elimu na mafunzo kwa wakulima kuhusu matumizi ya teknolojia za kisasa kwenye kilimo.

Wakulima hao watanufaika na teknolojia hizo itakayowaunganisha na mnyororo wa thamani ya mazao ni kutoka mkoa Morogoro, Pwani, Dar es Salaam ,Tanga na Iringa.

Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk Geofrey Mkamilo alisema hayo wakati akimbaribisha Mkuu wa wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro, Mathayo Masele aliyemwakilisha mkuu wa mkoa huo , Martine Shigella , kuzundua Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo .

Dk Mkamilo alisema , kituo hicho kitatoa mafunzo mwaka mzima kwa wakulima na kitakuwa na wataalamu mbalimbali wa kilimo wakiwemo watatifi na wataalaamu wa huduma za ugani.

“ TARI iko tayari kuhakikisha ina leta mapinduzi ya kilimo na kuhamasisha wakulima kuachana na kilimo cha mazoea walichokuwa wanalima babu na bibi zetu “ alisema Dk Mkamilo.

Hata hivyo alisema , katika kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji nchini, Taasisi imekuwa ikifanya kazi na Taasisi zingine ikiwemo ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu (TOSCI) , Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) na Makampuni mengine ya uzalishaji na usambazaji wa mbegu nchini.

Dk Mkamilo alisema , pia ina ratibu shughuli za utafiti na uhamasishaji wa matumizi ya teknolojia za kilimo na ubunifu kwa lengo la kuongeza tija.

Pia ina wafundisha wakulima kuhusu matumizi teknolojia za mbegu za kisasa ambazo zinapambana na magonjwa,mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuongeza uzalishaji .

Dk Mkamilo alisema, pamoja na kuonyesha teknolojia ya mbegu hizo ambazo zimefanyiwa utafiti wa kutosha katika mikoa mbalimbali pia watafiti wa Taasisi hiyo wamekuwa wakiwaonesha wakulima kutumia mbinu bora za kilimo pamoja na njia za kutumia vidhibiti magonjwa.

Naye Mkurugenzi wa kituo cha TARI Mlingano, Dk Catherine Senkoro alisema ,katika kituo hicho wakulima watapata fursa ya kujifunza kujua matumizi ya udongo kulingana na mazao wanayokusudia kulima katika maeneo mikoa yao ikiwemo fursa ya kupimwa kwa udongo wa shamba na kupewa ushauri .

Dk Senkoro alisema ,wakulima hao watafundishwa jinsi ya kuyatumia mazao ya mikundekunde na fiwi ambayo yanauwezo mkubwa wa kuchanganywa na mazao mengine na kuongeza mboji katika udongo pamoja na kudhibiti magonjwa ya minyoo na magugu.

“ Mkundekunde kwenye shamba a migomba pia inasaidia kuondoa ugonjwa wa minyoo kwenye migomba ambayo imekuwa ikisababisha uzalishaji kupungua” alisema Dk Senkoro.

Kwa upande wake Mratibu wa kituo cha Utafiti TARI Mikocheni,Dk Fred Tairo alisema ,wameanzisha teknolojia ya kuzalisha mbegu kwa kutumia tishu (chupa) kwa mazao ya Migomba, Mananasi ,Viazi vitamu,Zabibu, Mihogo,Vanila na Mkonge ambazo hazipati magonjwa na kuongeza uzalishaji ukilinganisha na mbegu zingine.

Mmoja wa wakulima waliofika kujifunza katika kituo hicho mahiri, Kinyemi Khatibu kutoka ya kata ya Mlimani Manispaa ya Morogoro alisema, amefurahishwa kwa kuanzishwa kwa kituo na kitamuwezesha kupata elimu ya kuboresha kilimo chake kuanzia namna ya kuandaa mashamba,upandaji na utunzaji pamoja na kuongeza thamani ya mazao ili kupata tija katika eneo dogo.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kituo hicho, Mkuu wa wilaya ya Malinyi , Masele aliiomba TARI kukitumia Kituo hicho kuwagundisha vijana namna ya uendeshaji wa kilimo Biashara ambazo kitakuwa ni ukombozi kwao . Pia alizitaka Halmashauri za wilaya za mkoa huo na mingine kukitumia kituo hicho kwa kuwapekea maofisa ugani ili waweze kuongezewa teknolojia za kisasa za kilimo ili wakautumie kuanzisha mashamba darasa katika maeneo yao kwa ajili ya wakulima waweze kupata elimu na maarifa ya uendeshaji wa kilimo cha kisasa kitakayowapatia tija.

 Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) , Dk Geofrey Mkamilo  ( mwenye kushika kisemeo ) akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro, Mathayo Masele  ( wa kwanza kushoto) ambaye akimwakilisha mkuu wa mkoa huo , Martine Shigella  , katika   uzinduzi wa Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo  Kanda ya Mashariki  kwenye  viwanja vya  Mwalimu J.K.Nyerere ( Nane Nane) vilivyopo mkoani humo  ambacho kitatumika kutoa elimu na  mafunzo  kwa wakulima kuhusu matumizi ya  teknolojia ya kisasa kwenye  kilimo.

Mratibu wa Utafiti wa zao la Miwa nchini, Dk Nessie Luambano ( kushoto) ,akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro, Mathayo Masele  ( wa pili  kulia )  aliyemwakilisha  mkuu wa mkoa huo , Martine Shigella katika   uzinduzi wa Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo  Kanda ya Mashariki,  juzi katika viwanja vya  Mwalimu J.K.Nyerere ( Nane Nane) vilivyopo mkoani humo  ambacho kitatumika kutoa elimu na  mafunzo  kwa wakulima kuhusu matumizi  ya teknolojia ya kisasa kwenye  kilimo ,(  wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI),Dk Geofrey Mkamilo.


Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) , Dk Geofrey Mkamilo  ( kati kati ) akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro, Mathayo Masele  ( wapili kutoka kushoto) ambaye akimwakilisha mkuu wa mkoa huo , Martine Shigella  , katika   uzinduzi wa Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo  Kanda ya Mashariki  kwenye  viwanja vya  Mwalimu J.K.Nyerere ( Nane Nane) vilivyopo mkoani humo  ambacho kitatumika kutoa elimu na  mafunzo  kwa wakulima kuhusu matumizi ya  teknolojia ya kisasa kwenye  kilimo. ( Picha na John Nditi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...