Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi kwa kutoa huduma za usafirishaji wa shehena ndani ya nchi na nje ya nchi.

Akizungumza na katika mkutano wa wadau wa usafirishaji wa shehena nje ya nchi, Mkurugenzi Udhibibiti Huduma za Bandari na Usafiri wa Meli wa TASAC Bw. Deogratius Mukasa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, amesema kuwa kuna umuhimu wa kuwajengea uwezo wasafirishaji wa shehena kwa kutoa elimu ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

Amesema kuwa, elimu hiyo ni endelelevu kwa wadau kwani baada ya kutolewa  jijini Dar es Salaam itatolewa pia katika mikoa ya Tanga na Arusha ili kuweza kuwapa elimu mawakala wa usafirishaji wa shehena za kwenda nje ya  nchi na zile za kuingia nchini.

Mukasa amesema TASAC inawasikiliza sana wadau, na hata inapounda kanuni huwashirikisha wadau ili kupata maoni yao.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu Shirika la Wasafirishaji wa Shehena ISCOS kutoka Kenya Bw. Daniel Kiangi amesema kuwa, Shirika hilo lina wanachama wanne ambao ni Tanzania, Kenya Uganda na Zambia. Vilevile wamekuwa na ushirikiano wa karibu na wadau wa  usafirishaji shehena kwa njia ya maji ikiwemo TASAC, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA), Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), n.k.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Wasafirishaji wa Shehena kwa njia ya Maji nchini Tanzania, Bw. Ashraf Khan amesema kuwa wasafirishaji wa mizigo kwa njia ya maji wanahitaji kuwa na elimu na sio kufanya biashara hiyo kiholela ili kuepuka changamoto mbalimbali ambazo wanaweza kukutana nazo.

Amesema kuwa tangu kuundwa kwa TASAC, changamoto mbalimbali zimeweza kutatuliwa kwa kuwa Baraza hili kwa kushirikiana na TASAC limeweza kuwasaidia wanachama wake kupunguza gharama kutokana na kujua taratibu zilizowekwa kwa wasafirishaji ndani na nje ya nchi, pamoja na kufanya kazi kwa weledi pande zote mbili za mdau na mdhibiti.

 

Mkurugenzi wa Udhibiti Huduma za Usafiri Majini wa Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) Deogratius Mukasa akizungumza katika mkutano wa wadau wa usafirishaji wa shehena wa ndani na nje nchi katika mkutano uliofanyika jijini Dar esSalaam.
Mkurugenzi Mkuu wa ISCOS Daniel Kiangi akizungumza kuhusiana na wadau kushirikiana katika masuala mbalimbali katika kujenga kwa ajili ya maendeleo katika mkutano wadau wa usafirishaji wa shehena ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya wadau wakifatilia mada katika mkutano wa wadau wa usafirishaji wa shehena Ndani na Nje ya nchi katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya wadau wa ushafirishaji wa shehena za ndani na nje ya nchi mara baada ya kufanya majadiliano katika sekta ya usafiri wa maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti wa Huduma za Usafiri Majini wa TASAC Deogratius Mukasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo kukutana na wadau wa usafirishaji wa shehena ndani ya nchi na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Baraza la Usafirishaji wa Shehena ndani na nje ya nchi Ashraf Khan akizungumza kuhusiana na ushirikiano na mamlaka za serikali katika kutimiza matakwa ya sekta a usafirishaji wa kwa njia ya maji katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.


 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...