Shirika
la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wafanyabiashara na wajasiriamali
nchini kujitokeza katika Maonesho ya biashara ya kimataifa ya 45
Sabasaba yanayotarajiwa kuanza Juni 28 katika Viwanja vya Maonesho vya
Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo katika
Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Masoko
(TBS) Bi.Gladness Kaseka amesema kuwa kutakuwa na huduma ambazo
watakuwa wanatoa papo hapo kulinganisha na maonesho ya kipindi
kilichopita kama huduma ya usajili wa majengo ya bidhaa za chakula na
vipodozi vitatolewa papo hapo
"Tutawapa msaada wa kujisajili
kwenye mfumo ambapo ilikuwa ni changamoto ambayo wamepitia kwa muda
mrefu tutawasaidia kujisajili kwenye mfumo pia tutawapatia mkaguzi
palepale na kuweza kwenda kukagua mazingira yao ya biashara na kuwapatia
kile kibari ndani ya siku moja". Amesema Bi.Gladness.
Aidha
Bi.Gladness amesema kipindi chote hicho cha Maonesho wafanyabiashara
wanaopeleka biashara na bidhaa nje ya nchi watapata huduma na taarifa
mbalimbali za masoko ya bidhaa zao ili kuepuka vikwazo vya biashara
wanapokua wakifanya biashara nje ya nchi.
Pamoja na hayo
Bi.Gladness amewataka wale ambao wanahitaji huduma za viwango kufika
katika maonesho hayo kwasababu kutakuwa na huduma za kuuza viwango
katika banda lao pia watatoa elimu kwa wadau mbalimbali wa viwango.
Home
HABARI
TBS KUFANYA USAJILI WA MAJENGO YA BIDHAA ZA CHAKULA NDANI YA SIKU MOJA KIPINDI CHA SABASABA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...