
*****************************
Unguja na Shinyanga wameongoza kwenye mchezo wa kurusha tufe kwenye mashindano ya Taaluma na Michezo kwa shule za Sekondari (UMISSETA) kwenye fainali ziolizofanyika leo Juni 26, 2021 mjini Mtwara.
Msemaji wa UMISSETA 2021, John Mapepele amesema Abdala Salum kutoka Unguja ameibuka kuwa mshindi wa kwanza baada ya kurusha umbali wa mita 14 na sentimita 30 akigfuatiwa na Edward Michaeli kutoka mkoa wa Dar es Salaam aliyerusha umbali wa mita 11 na sentimita 97 wakati nafasi ya tatu imechukuliwa na Rajabu Mtonyi kutoka Mkoa wa Dodoma aliyerusha umbali wa mita 11 na sentimita 47.
Kwa upande wa wasichana Keflonia Daudi kutoka Mkoa wa shinyanga ndiye Msindi wa kwanza kwa kurusha mita 8 na sentimita 93 akifuatiwa na Martha Matinga kutoka Simiyu aliyerusha umbali wa mita 8 na sentimita 88 ambapo nafasi ya tatu ilichukuliwa na Fatma Saidi kutoka Unguja aliyerusha umbali wa mita 8 na sentimita 70.
Kwa upande wa soka msimamo wa ligi ni kama unavyoonekana kwenye jendwali hapo chini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...