Leo Julai 2, 2021 wadau mbalimbali wametembelea Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) . Kupitia maonesho hayo, GST imeendelea kuwaelimisha na kuwafahamisha juu ya masuala mbalimbali ikiwemo aina za madini na miamba inayopatikana katika maeneo mbalimbali ya nchi; huduma zitolewazo na GST; na njia za kisayansi zinazotumika katika utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji Madini.

Aidha, katika msimu huu wa Sabasaba GST inatoa huduma za utambuzi wa madini kwa kutumia vifaa vya kisasa vilivyopo katika Banda lake. Pia, ushauri wa namna bora ya kutafuta na kuchenjua madini unatolewa . Vilevile, Banda la GST linaonesha madini mbalimbali yanayopatikana nchini ikiwa pamoja na Madini pekee ya Tanzanite.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...