PATRICIA KIMELEMETA

TAASISI ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imewataka wajawazito kuacha kula udongo wa Pemba kwa sababu una viambata vya sumu ambavyo vinaweza kuhatarisha afya ya mtoto angali tumboni na kuzaliwa wakiwa na uzito mdogo(njiti)wafu au kwenye hitilafu za kimaumbile.

Akizungumza hivi karibuni Mkoani Dar as Salaam,  Ofisa Mtafiti Mwandamizi wa TFNC, Neema Joshua amesema kuwa, wajawazito wengi wanapenda kula udongo bila ya kujua madhara yake, hivyo basi wanapaswa kubadilika na kuacha mara moja ili wasiweze kuathiri afya ya ukuaji wa mtoto kuanzia tumboni hadi anapozaliwa.

Amesema kuwa, tafiti mbalimbali zilizofanywa na wadau wa afya kutoka ndani na nje ya nchi umebainisha kuwa, udongo huo una viambata vya sumu ambayo vinaweza kuleta madhara kwa mjamzito na mtoto wake,hali ambayo itadhohofisha au kuhatarisha kabisa ukuaji wa mtoto kuanzia utombini.

"Tunawashauri wajawazito wasitumie udongo wa Pemba kabisa, kwa sababu una viambata vya sumu ambayo vinaweza kusababisha kujifungua watoto njiti, wafu au kwenye hitilafu ya kimaumbile," amesema Joshua.

Amesema kuwa, ukuaji wa mtoto unaanzia tumboni kwa mama yake hadi anapozaliwa na kuendelea kunyonya maziwa ya mama hadi anapotimiza miezi sita na kuanzia kula vyakula mchanganyiko ambavyo vinasaidia katika malezi na makuzi ya mtoto.

Amesema kuwa, hivyo basi wajawazito wanapaswa kula vyakula vyenye virutubisho pamoja na kusimamia malezi ya watoto wao kuanzia tumboni ili wasiweze kuwaathiri kwa namna moja au nyingine.

" Malezi na makuzi ya mtoto yanaanzia tumboni kwa mama yake,hivyo basi mjamzito anapaswa kula vyakula vyrnye virutubisho vyote ili kuhakikisha anaimarisha afya ya mtoto wake mpaka atakapojifungua,"amesema.

Ameongeza kuwa, mkakati wa TFNC ni kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi hasa wanawake na wajawazito wanaotumia udongo kuacha mara moja ili kuepusha madhara yatokanayo na udongo huo.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...