Na PATRICIA KIMELEMETA

MZAZI au mlezi anatakiwa kumpeleka mtoto hospitali ili aweze kupatiwa dawa ya Vitamin A ambayo yanasaidia kuimarisha afya ya mtoto kuanzia miezi sita hadi miezi 59.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika hivi karibuni, Ofisa Lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lish(TFNC),,Neema Joshua amesema kuwa, mtoto anapotimiza miezi sita,anapaswa kupewa dawa za Vitamin A huku ikienda sambamba kwa kumuanzishia vyakula mchanganyiko kwa kuzingatia makundi matano ya vyakula kwa ajili ya kuimarisha afya yake.

Ameyataja makundi hayo ni pamoja na wanga,nyama, mbogamboga, jamii ya mikunde na matunda.

Amesema, mtoto wa miezi sita hana uwezo wa kutafuna nyama, hivyo basi mzazi au malezi unapaswa kumsagia ili aweze kula bila ya kupata matatizo yoyote pamoja na kumkamulia matunda na kumnywesha.

"Wazazi wengine au walezi wanadhani kuwa watoto wa miezi sita hawezi kula nyama kwa sababu hana meno, kitu hicho sio kweli,wanapaswa kumsagia kwa namna yoyote ile na kumlisha ili asipate usumbufu wowote,, kwa sababu nyama ni muhimu kwa kuimarisha afya ya mtoto" amesema Joshua.

Ameongeza kuwa, malezi na makuzi bora ya mtoto yanaanza tangu akiwa mchanga ikiwa ni pamoja na mzazi au mlezi kuzingatia mlo kamili wa mtoto ambayo utajumuisha makundi matano ya chakula,lengo ni kuimarisha afya yake pamoja na kumuepusha na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuhatarisha afya yake.

Amesema kuwa, lakini pia, watoto hao wanapaswa kuendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa sababu yana lishe bora kwa mtoto ambayo yatamsaidia kukua vizuri huku akiendelea kula vyakula mchanganyiko.

"Mtoto anapotimiza miezi sita anatakiwa kula vyakula vyote kwa kuzingatia makundi matano ya vyakula hata kama hana meno,kinachotakiwa ni mzazi au malezi kumrahisishia ulaji wake ili aweze kula vizuri bila ya usumbufu wowote," amesema.

Alisema kutokana na hali hiyo, wazazi au walezi wanashauriwa kuzingatia ushauri unaotolewa na watalaam wa afya ili waweze kuwalea watoto wao katika mazingira bora na salama.

Ameongeza kuwa, TFNC itaendelea kushirikian na wadau mbalimbali ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya malezi na makuzi bora kwa mtoto hali ambayo itasaidia kumuepusha na magonjwa mbalimbali.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...