PATRICIA KIMELEMETA


WAJAWAZITO wanaovuta sigara wanapaswa kuacha mara moja kwa sababu wanahatarisha maisha yao na watoto kuanzia tumboni.

Hayo yamesemwa na Ofisa Lishe Mtafitii kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania(TFNC), Adela Twin'omujuni kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika hivi karibuni Mkoani Dar es Salaam ambapo amesema kuwa, uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya mama mjamzito na mtoto.

Twin'omujuni amesema kuwa kuwa, malezi na makuzi ya mtoto yanaanzia tumboni kwa mama yake, hivyo basi mjamzito anapaswa kula vyakula bora kwa kuzingatia makundi yote matano ya vyakula lishe, ambayo ni pamoja na jamii ya kunde, wanga, matunda, nyama na mbogamboga.

Amesema kuwa, lengo bi kuimarisha afya ya mama mjamzito pamoja na mtoto wake ili anapozaliwa aweze kuwa na afya bora ambayo itamsaidia kumkingana magonjwa mbalimbali yakiwamo Yale ya kuambukiza na yasiyoambukiza.

Amesema kuwa, hivyo basi mjamzito anapaswa kuwahi kliniki ili aweze kupewa elimu  na watalaam wa afya ya kujilinda na magonjwa hayo pamoja na kumkinga mtoto wake kuanzia tumboni  ili  aweze kujifungua salama na mtoto mwenye afya

"Uvutaji wa sigara kwa mama mjamzito ni hatari kubwa ambayo inaweza kumuathiri yeye na mtoto wake kuanzia tumboni, hivyo basi mjamzito ambaye awali alikua anavuta sigara,anapaswa kuacha mara moja na kufuata maelekezo yanayotolewa na watalaam wa afya ili aweze kumlinda mtoto aliyepo tumboni," amesema Twin"onujuni.

Ameongeza kuwa, uvutaji wa  sigara unaua watu zaidi ya milioni 8 Duniani kote,ambapo kati yao milioni saba ni wale wanaovuta moja kwa moja na milioni 1.2 ni wale wanaokaa karibu na wavutaji wa sigara(kuvuta moshi wa sigara).

"Mjamzito anapaswa kwenda kliniki ili kupata elimu ya kutoka kwa watalaam wa afya ya umuhimu wa kumlinda mtoto kuanzia tumboni kwa mama yake hadi anapozaliwa na kutimiza miaka mitano, lengo ni kuhakikisha kuwa, huyo mtoto anapozaliwa anapata makuzi bora na salama kwa afya yake pamoja na kulishwa vyakula vya kumjenga na kumlinda mwili wake," amesema.

Amesema kuwa, sio sigara peke yake, mjamzito anapaswa kuacha kutumia aina yoyote ya dawa ya kulevya, pombe,Michele mbichi au udongo kwa sababu ni hatari kwa afya yake na mtoto pia.

Amesema hivyo basi anapaswa kupata muda mwingi wa kupumzika pamoja na kjzingatia mlo kamili kwa ajili ya kujilinda yeye mwenyewe pamoja na kumlinda mtoto.

Ameongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, TFNC itaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuzingatia matumizi ya chakula bora kwa kuzingatia makundi yote matano.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...