Wananchi wa Kigambo mkoani Dar es Salaam wakiwa kwenye kampeni ya Kampuni ya JATU PLC ya kuhamasisha wananchi kununua hisa za kampuni hiyo ambayo lengo lake ni kuwaokomboa kiuchumi
wasanii wakitoa burudani kwa wananchi wa Kigamboni wakati Kampuni ya JATU ikitoa elimu kuhusu hisa za kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwahamasisha wananchi kununua na hatimaye kupata gawio kila mwaka

Na Mwandishi Wetu

WANANCHI wachagamkia hisa za JATU!Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya wananchi wa Kigamboni mkoani Dar es Salaam kuendelea kuchangamkia kununua hisa za Kampuni ya Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini( JATU) ambazo lengo lake ni kuwakomboa kiuchumi.

Kampuni ya JATU ipo katika kampeni ya  kuhamasisha wananchi kununua hisa kwa lengo la kujikomboa kiuchumi huku wananchi hao mbali ya kununua hisa za kampuni hiyo wamepongeza ubunifu huo.

Wakizungumza baada ya kupata elimu inayohusu faida za kununua hisa za JATU wananchi hao wa Kigamboni wamesema ni wakati muafaka kwao kuwa sehemu ya wanaomiliki hisa za kampuni hiyo ambayo hisa moja inauzwa Sh.500 na ili ujiungeunatakiwa kununua hisa 10 ambayo thamani yake bi Sh.5000.

Mkazi wa Kigamboni Omari Majimarefu amesema kuwa amefurahishwa na maelezo ambayo yametolewa na maofisa wa JATU PLC na hivyo ameona ni vema akanunua hisa kama sehemu ya kujikomboa kiuchumi kwani, kupitia hisa alizonunua atapiga hatua kwenye shughuli zake za kujitafutia riziki kupitia bishara ndogondogo anazozifanya ndani ya Wilaya ya Kigamboni.

"Nilikuwa nasikia tu kuhus hisa za JATU PLC bahati nzuri sasa wamefika kwenye Wilaya ya Kigamboni, tumewasikiliza maofisa wao , na kwa kweli nimeona nina kila sababu ya kununua hisa , faida zake ni nyingi sana hasa kwa mtu ambaye anataka kujikomboa kiuchumi,"amesema Majimarefu.

Akifafanua zaidi Jonasi Mwandegere amesema kampuni ya JATU PLC imekuwa na kampeni nzuri ambayo kimsingi inakwenda kubadilisha maisha ya watu, kwani kwa anayenunua hisa za kampuni hiyo anakuwa na uhakika wa kuongeza mtaji wake kupitia fedha atakayopata kutokana na hisa alizonazo.

Aisha Binda ambaye ni mama lishe katika eneo hilo la Kigamboni ameeleza kuwa huu ni wakati wa akina mama ndani ya Wilaya hiyo kuhakikisha wananunua hisa za kampuni ya JATU kwani  imezingatia zaidi kumkomboa mwanamke kutokana na hisa za kampuni hiyo kuwa rafiki kwa wajasiriamali.

Wakati huo huo maofisa wa JATU PLC waliokuwa katika Wilaya ya Kigamboni wamesema wamefurahishwa na namna ambavyo mamia ya wananchi wamejitokeza kununua hisa za kampuni yao na kubwa zaidi ambao wanaahidi ni kuhakikisha wanashirikiana nao katika kuwaokomboa kiuchumi.

Wamefafanua hisa moja ya  JATU inauzwa Sh.500 tu, na mwananchi ili kujiunga anatakiwa kununua hisa 10, ikiwa na maana ya Sh. 5,000 na kila mwisho wa mwaka anapata gawio kwa faida ikizingatiwa hisa za kampuni yao zipo kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.

Aidha uwekezaji wa kampuni hiyo upo katika kilimo cha kisasa cha mashamba makubwa ya nafaka, matunda pamoja na biashara mbalimbali za mazao katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

"Endeleeni kununua hisa za JATU PLC leo, au mnunulie uupendaye , kumbuka kwamba unapokuwa na hisa utapata gawio la faida kila mwaka na pia hisa ni dhamana , pia n mlango wa kushiriki kilimo cha kisasa na kuwa wakala wa bidhaa za JATU na zaidi utapata mikopo yenye riba nafuu kutoka JATU Saccos,"amesema Mohamed Simbano ambaye ni Meneja wa JATU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...