Sehemu ya Bonde Dogo la Mto Mgolole ambalo lipo katika kata ya Kingolwira mkoani Morogoro, ambapo Jumuiya ya Watumia maji katika eneo hilo imeamua Kuachana na Ukataji miti hovyo na Uchomaji Mkaa ili Kukilinda chanzo hicho cha maji kwa kufanya Shughuli Mbadala ya Ufugaji Nyuki.

Kutoka kulia Afisa mkuu maendeleo ya Jamii kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu akipata maelezo kutoka Kwa Vongozi wa Jumuiya ya Watumia Maji katika Bonde Dogo la Mto Mgolole lililopo Katika Kata ya Kingolwira mkoani Morogoro, Jumuiya hiyo imeachana na Suala la Ukataji Miti hovyo na Uchomaji Mkaa na kuanza Shughuli ya Ufugaji Nyuki ili kulinda na kuhifadhi mazingira ya eneo hilo.



Baadhi ya Mizinga ya nyuki ambayo imekabidhiwa kwa Jumuiya ya Watumia Maji Katika Bonde Dogo la Mto Mgolole, ikiwa ni mbadala wa kufanya Shughuli zisizoharibu Mazingira kwa lengo la Kutunza na Kuhifadhi chanzo hicho cha maji.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watumia Maji Bonde Dogo la Mto Mgolole, Kobelo Kobelo akionesha moja ya Mzinga wa nyuki ukiwa ni Miongoni mwa mizinga iliyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa Jumuiya hiyo kuweza kufanya Shughuli mbadala isiyoharibu vyanzo vya maji ili kutunza Mazingira.



Baadhi ya Maofisa wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/ Ruvu wakiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Watumia Maji katika Bonde Dogo la Mto Mgolole, lililopo Kata ya Kingolwira mkoani Morogoro.

Na Mwandishi wetu, Morogoro
WANANCHI katika Kata ya Kingolwira na Bigwa mkoani Morogoro, wameamua kujielekeza katika Shughuli za Ufugaji wa Nyuki na kuachana na kazi ya Ukataji miti hovyo na Uchomaji mkaa ili kulinda na kuhifadhi Mazingira hususani kwenye Chanzo cha Maji katika Bonde Dogo la Mto Mgolole.

Bonde Dogo la Mto Mgolole ni miongoni mwa vyanzo vya maji, ambavyo awali vilikuwa hatarini kuharibiwa kwa sababu ya kuingiliwa na Shughuli za Kibinadamu.

Kufuatia hali hiyo Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeamua kuiwezesha Jumuiya ya Watumia maji Mgolole kufanya Shughuli za Ufugaji Nyuki kwa kuipatia mizinga, ikiwa ni hatua mbadala ya kuwaingizia Kipato Wananchi wa kata za Kingolwira na Bingwa.

Afisa Mkuu wa maendeleo ya Jamii wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Halima Faraji amesema Jumuiya ya Watumia maji Mgolole, imeipa kisogo Shughuli ya Ukataji miti hovyo, Uchomaji mkaa na ufyatuaji tofali ili kulinda mazingira hususani kwenye chanzo hicho cha maji.

"Kwa hiyo Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu, imeona mwitikio mkubwa wa Wananchi, Sasa wanaelewa Sheria na taratibu zinazo simamia Suala la utunzaji na uhifadhi wa Rasilimali maji" alisema Halima Faraji.

Baadhi ya Wananchi katika Kata hizo mbili akiwemo Kobelo Kobelo na Pepetua Kessy, wamesema Suala la Ufugaji nyuki limekuwa na tija kwao, kwa sababu licha ya kupata kipato cha Kujikimu lakini Wameweza Kulinda mazingira na Kuhifadhi Chanzo cha maji Katika Bonde hilo Dogo la Mto Mgolole.

“Tutakuwa wanyimi wa Fadhila, tusipotoa Shukrani zetu kwa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, kwa kutuwezesha kuwa wafugaji wa nyuki kwa Sababu tumepata faida kubwa na uelewa wa kutosha kuhusu mazingira, na kama Jamii tunapaswa kulinda Rasilimali maji na Mazingira” Walieleza Wananchi hao.

Ili kulinda Mazingira hususani vyanzo vya maji, Siku ya Mazingira Duniani iliyoadhimishwa June 5 mwaka huu, ililenga kuhamasisha Jamii kutumia nishati mbadala ili kuongoa mifumo Ikiolojia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...