Wataalam kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Ardhi (Land Administration Unit) wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa serikali za mitaa, vijiji, kata na Tarafa, Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na Kilwa Mkoa wa Lindi baada ya mafunzo ya sheria ya matumizi ya ardhi.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia mafunzo hayo.
Dk. Hidaya Kayuza kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Ardhi Chuo Kikuu Ardhi (ARU), akitoa mada kwenye mafunzo viongozi wa serikali za mitaa, vijiji, kata na Tarafa, Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na Kilwa Mkoa wa Lindi kuhusu sheria ya matumizi ya ardhi.

Na Mwandishi Wetu
WATAALAM kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Ardhi (Land Administration Unit) wa Chuo  Kikuu Ardhi wametoa mafunzo ya kujenga ufahamu kuhusu sheria ya matumizi ya ardhi kwa viongozi wa serikali za mitaa, vijiji, kata na Tarafa, Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na Kilwa Mkoa wa Lindi.

Mafunzo hayo yamelenga kujenga uelewa wa Sera na sheria sera za ardhi, haki ya kumiliki ardhi kwa wananchi pamoja na utatuzi wa migogoro ya ardhi ili  kuwasaidia katika usimamizi wa ardhi na  kukabiliana na changamoto za migogoro ya ardhi.

Mafunzo hayo yametolewa leo Julai 13, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ya Halmashauri ya Mtama  kwa  kufunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama,  Samwel Warioba Gunzar .

 Washiriki wa mafunzo hayo  walisikiliza mada zilizowasilishwa na kujadili kwa pamoja. Pia washiriki  walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu masuala ya Ardhi huku wakieleza pia changamoto wanazopitia katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wataalam walioshiriki kwenye kutoa mafunzo ni Dk. Hidaya Kayuza na Dkt. Fredrick Magina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...