Benki ya NBC nchini Tanzania, imeendelea kuwa kinara kwa mara ya nne mfululizo katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, yaliyohitimishwa jana katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar  es Salaam kwa kutwaa tuzo mbalimbali ikwemo ya ushindi wa kwanza katika kundi la taasisi za  Fedha zilizoshiriki maonesho hayo.

Pamoja na kuwa mdhamini mkuu wa Maonesho hayo benki hiyo ilikuwa mstari wa mbele katika kufanikisha ushiriki wa wadau wake mbalimbali katika maonesho hayo wakiwemo wajasiriamali, sambamba na kudhamini Kliniki ya biashara iliyoandaliwa kwa ushirikiano Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Akizungumza kwenye hafla ya ufungaji wa maonesho hayo Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja wadogo na wa kati kutoka Benki ya NBC, Bw Elvis Ndunguru alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye maonesho hayo umekuwa na tija kubwa kwa kuwa wamepata nafasi ya kuhudumia wateja wao sambamba kufungua fursa mpya za ushirikiano na taasisi mbalimbali likiwemo Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).

“Mbali na kushirikiana na taasisi zaidi ya 16 katika kufanikisha kliniki ya biashara kwenye maonesho haya, tumefanikiwa kufungua milango  na taasisi nyingine zinazohudumia wajasiriamali na wafanyabiashara wanaochipukia ikiwemo SIDO ili tuweze kuona namna ambavyo tunaweza kuunganisha nguvu ili kwa pamoja tuwahudumie wadau hao muhimu kwenye ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara,’’ alisema.

  Aliongeza kuwa wakiwa kwenye maonesho hayo benki hiyo ilipata fursa ya kupokea wageni mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Makamu wa Rais  Dk Phillip Mpango aliezindua maonesho hayo, mawaziri mbalimbali pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mh Hemed Suleimani Abdulla ambao pia waliiopongeza ipongeza benki hiyo kwa namna inavyoshiriki kuwasaidia wafanyabiashara nchini.

“Kama benki tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba tunayafanyia kazi maoni yote yaliyotolewa na viongozi waandamizi wa serikali pamoja na wateja wetu waliotutembela lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba tunakusanya maoni yatayatuwezesha kubuni huduma zinazoendana na matarajio yao,’’

 “Benki ya NBC tumeendelea kuwa karibu na wafanyabiashara wa kati (SMEs) na ndio maana tumezidi kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji yao kama vile mikopo ya bila dhamana kwa wazabuni na wasambazaji wa bidhaa, huduma za kidigitali zinazookoa muda pamoja na gharama nafuu zaidi za uendeshaji ili kuongeza tija kwenye biashara zao,’’ alisema.

 Akizungumzia kuhusiana na ushirikiano mpya baina ya benki hiyo na taasisi yake, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Mhand. Prof. Sylvester Mpanduji aliishukuru benki hiyo kwa kufungua milango ya kimahusiano na taasisi hiyo huku akibainisha kuwa inaonyesha wazi nia ya benki hiyo kuleta mapinduzi ya kihuduma kwa kusaidia sekta ya viwanda na biashara.

“Ushirikiano huu mpya na benki ya NBC unadhihirisha nia ya benki hii katika kuinua na kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati. SIDO tunakaribisha vyema mahusiano haya mapya na tupo tayari kushirikiana na benki kwa mustakabari mzima wa ustawi wa sekta ya viwanda vidogo na wafanyabiashara nchini,’’ alisema.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo kwa wateja binafsi Benki ya NBC Bw Abel Kaseko akionyesha tuzo ya ushindi baada ya benki hiyo kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za  Fedha kwa mara ya nne mfululizo katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, yaliyohitimishwa jana katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar  es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Mh Hemed Suleiman Abdulla (wa pili kulia – meza kuu) na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kushoto –meza kuu).

Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Mh Hemed Suleiman Abdulla (wa pili kushoto) akipata maelezo kuhusu huduma za Benki ya NBC kutoka kwa Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki hiyo, Bw Jonathan Bitababaje (kulia) wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya biashara ya Sabasaba yaliyohitimishwa jijini Dar es Salaam jana. Wanaofuatilia maelezo hayo pia ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (katikati) na Mkurugenzi wa Tantrade balozi Mteule Edwin Rutageruka (kushoto). Benki ya NBC  ndio ilikuwa mdhamini mkuu wa Maonesho hayo.

 


Wafanyakazi wa benki ya NBC wakijipongeza baada ya kutwaa tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo za ubunifu, kutoa huduma na bidhaa bora kwenye maonesho ya Sabasaba.

Muonekano wa tuzo hizo

Maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja wadogo na wa kati wa benki hiyo, Bw Elvis Ndunguru (Katikati)  wakipata maelezo kuhusu bidhaa zinazozalishwa na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)kutoka kwa mtaalamu wa mitambo wa SIDO- Kilimajaro Bw Boniventure Shayo (wa pili kushoto) pamoja na Meneja Masoko SIDO Makao Makuu Bi Lilian Massawe (kushoto) wakati maofisa hao walipotembelea banda la SIDO lililopo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, yaliyohitimishwa jana katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar  es Salaam.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja wadogo na wa kati wa benki ya NBC, Bw Elvis Ndunguru (Kushoto)  akipokea zawadi ya bidhaa za chakula kutoka kwa mmoja wajasiriamali wa bidhaa za kusindikwa Bi Flora Sumaye ikiwa ni ishara ya shukrani kutoka kwa mjasiriamali huyo kwenda benki ya NBC baada ya benki hiyo kumuwezesha na kudhamini ushiriki wake kwenye maonesho hayo.


 Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja wadogo na wa kati wa benki ya NBC, Bw Elvis Ndunguru (Kushoto)  pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bi. Neema Rose Singo wakiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa kitanzania walipotembelea banda la SIDO kwenye maonesho hayo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...