Muonekano mpya wa jina na nembo mpya ya Benki ya Serikali ya biashara 'Tanzania Commercial Bank' (TCB.)

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki mpya ya Serikali ya biashara  TCB na kueleza kuwa kinachotegemewa ni ubunifu na kufanya kazi kwa ushindani ili kujenga uchumi imara wa taifa, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TCB Sabasaba Moshingi  akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo na kuahidi kufanya kazi kwa kwa uadilifu ili kuyafikia malengo kwa hali ya juu, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa benki ya TPB na sasa TCB Edmund Mndolwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo na kusema kuwa taasisi hiyo ya umma itatoa huduma zote za kibenki kwa ubunifu na ushiundani, Jijini Dar es Salaam.









Matukio mbalimbali katika hafla hiyo ya uzinduzi.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV


 * Waziri Mwigulu azishauri benki kupunguza riba

* Afafanua suala la ufilisi wa dhamana kwa wateja

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amezindua rasmi benki ya  Serikali ya Biashara 'Tanzania Commercial Bank' (TCB,) ambayo ni muunganiko wa benki ya  Maendeleo (TIB)na  benki ya Posta (TPB) huku lengo kuu likielezwa ni kuundwa kwa benki kuu ya Serikali na ushindani ambayo itatoa huduma zote za kibenki na biashara kama benki nyingine za kibiashara duniani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri Nchemba amesema benki hizo zimeunganishwa kwa kuzingatia ushauri na matakwa ya kisheria hivyo wafanyakazi wa benki hiyo mpya hawana budi kulitendea haki kwa jina  hilo kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii, ushindani na ubunifu wa hali ya juu na kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji, kimfumo na taswira ya kuhimili ushindani wa kibiashara katika sekta ya fedha.

Amesema, benki hiyo itahudumia wateja  wote na wafanyabashara waliokuwa TPB na TIB na itatoa huduma kwa viwango vya kuhakikisha mageuzi zaidi yanaendelea katika sekta ya fedha nchini ili kujenga uchumi imara na shindani katika viwango vya kimataifa.

" Hizi ni jitihada za Serikali katika kujenga uchumi wa taifa kwa kuzingatia uadlifu na ubunifu na sisi Wizara ya fedha na benki kuu tutatoa ushirikiano katika kuijenga benki ya biashara ya Serikali nchini TCB.'' Amesema Mwigulu.

Aidha Waziri Nchemba amezishauri benki zote nchini kushusha riba katika hatua zilizopo mikononi mwao na hiyo ni pamoja na kuangalia namna wanavyofilisi mali za wateja pindi wanaposhindwa kurejesha mikopo yao.

"Baadhi ya madalali wamekuwa wakiendesha minada ya dhamana za wateja kitapeli, mteja anaweza kuwa amelipa asilimia 95 ya mkopo na kubaki asilimia 5 pekee....hapa baadhi ya madalali wasio waaminifu wanauza dhamana kwa mnada ambao unazidi fedha iliyobaki, huu ni utapeli."  Amesema.

Pia Mwigulu amewashauri wananchi kutumia fursa za uwepo wa mabenki na kuacha tabia ya kukwepa mifumo rasmi ya fedha na kutumia mifumo isiyo rasmi ikiwemo kukopa sehemu za riba ya juu pamoja na masharti magumu yasiyoweza kuhimili kupitia biashara.

Awali Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa benki TPB na sasa TCB Sabasaba Moshingi amesema kuanzishwa kwa benki hiyo ya biashara ya Serikali ni muhimu sana katika kujenga uchumi imara na shindani pamoja na kuimarisha sekta ya fedha.

Moshingi amesema, Benki kuu ya Tanzania (BOT,) pamoja na Wizara ya Fedha imesimamia mageuzi hayo na kuahidi kufanya kazi kwa uadilifu katika kujenga uchumi imara wa taifa.

Vilevile amesema, benki hiyo ikiwa taasisi ya umma itatoa huduma kwa wateja wote kuanzia ngazi ya chini kulingana na mahitaji yao.

Serikali imeendelea kuunganisha taasisi zake zinazofanya kazi zinazofanana ili kuimarisha ufanisi na ushindani zaidi, Benki ya Biashara ya Serikali (TCB,) ni zao la benki ya Posta (TPB) na benki ya Maendeleo (TIB.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...