MBUNGE wa jimbo la Mchinga  Salma Rashid Kikwete amefanya ziara kwenye kata ya Kiwawa ambapo amefanya mikutano ya hadhara kijiji cha Kiwawa na Mputwa.

Mheshimiwa Salma Kikwete ameendelea kuwasisitiza wananchi wa Kiwawa kuchapa kazi na kuwa na imani na serikali yao inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwani tayari serikali imeshatenga pesa nyingi kwaajili ya miradi ya maendeleo na huduma za jamii ikiwemo huduma ya maji, afya na elimu pamoja na ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano ya simu,  umeme wa REA na barabara kupitia mfuko TARURA na changamoto nyingine za vijana, wanawake na walemavu kama vile mikopo ya halmashauri.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiwawa amewahakikishia kuwa zaidi ya Milioni 180 imetengwa kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara ya kutoka Milola kufika Kiwawa pamoja na huduma ya mawasiliano ya simu tayari ujenzi wa mnara wa simu wa TTCL unaendelea kijiji cha Mputwa. Pia, Mhe. Salma Kikwete amepokea changamoto za wananchi kama vile kuchelewa kwa mikopo ya pembejeo, miundombinu ya barabara na mawasiliano ya simu katika maeneo hayo na kuahidi kutoa ushirikiano kuzishughulikia.

Akiwa njiani kuelekea kata ya Kiwawa Mbunge amejionea kero kubwa ya barabara inayokabili kata hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...