Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la wajumbe wa CEOrt ambao ni maofisa watendaji wakuu wa taasisi mbalimbali za sekta binafsi na kujadili ni jinsi gani sekta binafsi zitashirikiana na mipango ya serikali ya maendeleo ya miaka mitano ijayo ya kukuza uchumi wa Taifa.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba (kushoto)  akizungumza na maofisa watendaji wakuu wa taasisi mbalimbali za sekta binafsi kwenye mkutano wao wakiwa wajumbe wa CEO Roundtable of Tanzania (CEOrt). Mkutano huu uliofanyika jijini Dar es Salaam ulilenga kuona jinsi gani sekta binafsi zinaweza kushirikiana na serikali katika kufanikisha mipango ya maendeleo ya miaka mitano ijayo ya kukuza uchumi wa Taifa. Kulia ni Mwenyekiti wa CEOrt,  Sanjay Rughani.

Mwenyekiti wa CEOrt, Sanjay Rughani akizungumza kwenye mkutano wa wajumbe wa CEOrt ambao ni maofisa watendaji wakuu wa taasisi mbalimbali za sekta binafsi uliofanyika jijini Dar es Salaam ukiwa na lengo la kuona jinsi gani sekta binafsi zitashirikiana na mipango ya serikali ya maendeleo ya miaka mitano ijayo ya kukuza uchumi wa Taifa. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe . Dkt Mwigulu Nchemba.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...