Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dorothy Gwajima amesema watanzania wanatakiwa kuwa na imani na chanjo ya uviko 19 iliyoletwa nchini kwani ni salama na imethibitishqa na Shirika la Afya duniani(WHO).

Ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa ya uzinduzi wa chanjo ya Kinga ya Uviko 19 utakaofanyika kesho kwa Rais wa Jamhuri ha Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu kuchanjwa.

Gwajima amesema, kesho Rais Samia atazindua chanjo hiyo kwakuwa mtanzania wa kwanza kuchanjwa baada ya Tanzania kupokea chanjo hizo kutoka nchini Marekani.


“Rais wetu ameonesha ushujaa na Utayari wake wa kuongoza utoaji wa chanjo ya Uviko 19  na hili tunalisema kama uthubutu na uzalendo kwa taifa lake,”amesema Gwajima.

Amesema, watanzania wanatakiwa kuwa na imani na chanjo hiyo kwani ni salama na inamtasaidia mwananchi kupambana na wimbi la tatu la ugonjwa huo ambao umeshika kasi duniani.

Amesema, Watakaoanza kupata chanjo ni makundi maalumu wazee kuanzia miaka 50, wagonjwa ndio wanaoshambuliwa na magonjwa kama kisukari, moyo na mengine

Gwajima amesema, serikali wamedhamiria Kuimarisha huduma ya elimu ya chanjo ya uviko 19 lengo likiwa ni kila mwananchi popote alipo apate elimu, kusikia  na kupata ufafanuzi wa kisayansi.

Amesema, Watakaoanza kupata chanjo ni makundi maalumu wazee kuanzia miaka 50, wagonjwa ndio wanaoahambuliwa

“Baada ya uzinduzi wa kesho wa Rais Samia utafuata wa kila mkoa itakayokuwa inaongozwa na wakuu wa mikoa na chanjo hizo zitatolewa kwa makundi maalumu,”amesema.

Naye moja ya wataalamu wa Kinga kutoka Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Prof Karim Premji Manji amewaondoa hofu watanzania kuwa chanjo iko salama, ingawa watu wamekuwa wanahoji muda wa kutengenezwa kwa chanjo hiyo.


“Chanjo inaweza kutengenezwa ndani ya muda mfupi, mambo yamebadilika na sayansi imezidi kubadilika hususani kwa magonjwa yanayoua haraka kama ebola, uviko na mengineyo,”amesema Prof Manji

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kinga katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Leonard Subi amesema Chanjo inaweza kutengenezwa ndani ya mwaka mmoja na inatengenezwa kuzingatia mfumo sahihi wa kisayansi.

Amewataka wananchi kuchanjwa kinga hiyo ili kumsaidia pia atakapopata maambukizi hayatakuwa makali na kumfanya kushindwa kwenda katika shughuli zake za kila siku.

Kufikia tarehe 22 Julai, 2021 jumla watu 4,127,963 walishapoteza maisha duniani huku 191,773,590 wakiwa wamethibitika kuwa na maambukizi ya UVIKO 19,   upande wa Afrika kwa tarehe hiyo hesabu ya walioambukizwa lishafikia 4,583,414 na vifo 108,056.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Doroth Gwajima(kulia) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu uzinduzi rasmi wa chanjo ya Corona ambayo itazinduliwa kesho Julai 28,2021 Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ataongoza Watanzania kwa kuwa wa kwanza kupata chanjo hiyo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Kinga katika Wizara hiyo Dk.Leonard Subi.
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya  Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (kushoto) akisisitiza jambo kuhusu chanjo ya Corona ambayo itatolewa kwa wananchi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuizindua rasmi kesho Julai 28,2021.Ametumia nafasi hiyo kuwatoa hofu wananchi kuhusu chanjo hiyo kwani nia ya Serikali ni kuwalinda watu wake.
Mtalaamu wa Kinga kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi(MUHAS) Profesa Karim Manji(kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Doroth Gwajima.Mkutano huo ulikuwa unazungumzia uzinduzi rasmi wa kutoa chanjo ya Corona kitaifa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Doroth Gwajima (kulia) akisisitiza jambo kwa Watanzania kuhusu chanjo ya Corona ambapo amesisitiza umuhimu wa wananchi kupata taarifa sahihi kuhusu chanjo hiyo na taarifa nyingine zote zinazohusu janga la Corona.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Doroth Gwajima akizungumza na watalaamu mbalimbali na viongozi wa Wizara hiyo baada ya kumaliza kikao chake na waandishi wa habari leo Julai 28, 2021.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...