WAKAZI wa Temeke wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya sabasaba mkoani Dar es Salaam na kununua hisa za kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umaskini (JATU,) ikiwa ni siku ya mwisho ya kununua hisa moja kwa gharama ya shilingi 500 pekee.

Akizungumza wakati wa kufunga zoezi hilo la kununua hisa leo mkoani Dar es Salaam Meneja wa kampuni ya JATU Mohammed Simbano amesema kuwa, kwa siku 45 wamekuwa wakizunguka katika maeneo mbalimbali nchini na kutoa elimu juu ya hisa pamoja na kuwahimiza wananchi kununua hisa ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Amesema kuwa kwa siku 45 walizofanya kampeni hiyo katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mingine ikiwemo Morogoro, Dodoma, Mwanza, Arusha na Mwanza na licha ya wananchi kupata elimu ya hisa pia wamepata kufahamu fursa zaidi za masoko, kilimo na viwanda zinazopatikana kupitia JATU PLC.

Aidha amesema kuwa wamejipanga katika kuwekeza katika kilimo cha kisasa na kuweza kuwakomboa wananchi wengi zaidi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliohudhuria hafla hiyo wameeleza kufurahishwa elimu ya fedha na kununua hisa kupitia kampuni hiyo na kuweka wazi kuwa ni fursa adhimu ya kumiliki hisa hizo kwa kununua hisa kumi kwa gharama ya shilingi 5,000.

Mkazi wa Mbagala kuu Shomari Masoud amesema amefurahushwa na  elimu inayotolewa na maofisa wa JATU na kuamua kununua hisa ili kuweza kujikomboa kiuchumi hasa katika biashara yake ya kuuza matunda.

Aidha Prica Joseph Mkazi wa  Chamanzi amesema alikuwa akisikia kuhusu JATU kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na leo amepata bahati ya kukutana na maofisa wa JATU PLC katika viwanja vya sabasaba na baada ya elimu hiyo ameona ni muhimu kununua hisa pamoja na kufahamu kuhusu fursa za kilimo, viwanda na masoko ambazo zitakazomsaidia  kujikimboa kiuchumi.

Licha ya kupata gawio pia hisa kutoka JATU pia ni mlango wa kushiriki shughuli za kilimo cha kisasa, wakala wa bidhaa za JATU na kupata mikopo yenye riba nafuu kutoka JATU Saccos.

Hafla hiyo iliongozwa na kupambwa na msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto maarufu kama 'mjomba' pamoja na vikundi mbalimbali vya sanaa.

JATU imefanya kampeni kubwa katika mikoa mbalimbali nchini katika kuhakikisha wanabadili maisha ya watu kiuchumi kwa kununua hisa na kupata dhamana na  gawio la faida kila mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...