Na Marco Maduhu, Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amezindua mradi wa maji wa kisima kirefu, katika shule ya Sekondari Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Zoezi la uzinduzi wa mradi huo limefanyika leo katika shule hiyo, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, na chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, wakiwamo wanafunzi na wananchi.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, amesema mradi huo utasaidia wanafunzi kutunza mazingira ya shule kwa kupanda miti, pamoja na usafi.

"Mpaka sasa nimechimba visima viwili vya maji katika shule za Sekondari, ya Mwawaza na hapa Kolandoto, ili kumaliza tatizo la wanafunzi kukosa maji shuleni, na hili nitalifanya kwenye shule zote ambazo zina changamoto ya ukosefu wa maji," amesema Katambi.

Aidha amewataka wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii, ili watimize ndoto zao, huku akiahidi kuzifanyia kazi changamoto zote katika shule hiyo, ikiwamo ya upungufu wa mtundu ya choo, Walimu, Viti, Meza, na Nishati ya umeme.

Nao baadhi ya wanafunzi wa Shule hiyo akiwamo  Magesa Rubinza na Salma Abdul, kwa nyakati tofauti wamesema mradi huo wa maji utakuwa mkombozi kwao, hasa katika utunzaji wa mazingira na usafi, na kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Pia wamesema mradi huo wa maji umewapusha kupoteza muda wa masomo kwa kufuata maji umbari mrefu, pamoja na kubeba maji kutoka nyumbani na kufika shuleni wakiwa wameshachoka, na kutokuwa makini na masomo.

Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu, amempongeza Mbunge Katambi kwa kazi nzuri ambayo anaifanya, ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa vitendo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kolandoto Deus Maganga, amesema mradi huo wa maji ni mkombozi katika shule hiyo, kwa utunzaji wa mazingira na usafi, na hata kuondoa adha ya wananchi ya ukosefu wa maji, ambao anaishi jirani na shule hiyo, ambapo wamekuwa wakiyatumia.

Amesema mradi huo ulianza kutekelezwa June 8 mwaka huu, na kukamilika June 12, kwa gharama ya Sh.milioni 20, kwa msaada wa Ofisi ya Mbunge Katambi, chini ya mfadhili Serving Friends International kutoka Arusha.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira,  mwenye Kofia,akikata utepe kuzinduz mradi wa maji wa kisima kirefu katika shule ya Sekondari Kolandoto.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, akipampu maji katika mradi wa kisima kirefu Shule ya Sekondari Kolandoto, mara baada ya kumaliza kuuzindua.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Kolandoto Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mradi wa maji wa kisima kirefu shuleni hapo ambao umezinduliwa na Mbunge Katambi.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, Patrobas Katambi , akizungumza katika shule ya Sekondari Kolandoto alipofika kuzindua mradi wa maji wa Kisima Kirefu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...