Na Marco Maduhu, Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri wa Nchi Ofisi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, amefanya mkutano wa hadhara Kata ya Kolandoto kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo leo kwenye mkutano wa hadhara, amesema amejipanga vyema kutekeleza ahadi zake kwa vitendo ambazo aliziahidi kwenye kipindi cha kampeni 2020.

Amesema kwenye Kata hiyo kuna changamoto mbalimbali ambazo amezisikiliza kutoka kwa wananchi, ikiwamo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji, umeme, afya, upimaji wa ardhi, pamoja na ucheleweshwaji wa malipo ya Penshine za wazee.

"Mimi sina siasa za porojo, siasa zangu ni kazi tu, nazani matunda mmeanza kuona ndani ya kipindi changu kifupi, na hadi kufikia miaka mitano, Shinyanga itakuwa na maendeleo makubwa," amesema Katambi.

"Sasa hivi tumeshatoka kwenye mchakato wa bajeti, na fedha nyingi tu zimeshatengwa kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo ya wananchi, ambapo katika Bajeti ya barabara kuna Sh. bilioni 1.5 zitatumika kwa barabara za ndani tu, tumpongeze Rais wetu Samia," ameongeza Katambi.

Aidha amesema katika utendaji wake wa Kazi, hata ogopa mtu yoyote, na ata hakikisha mradi wa machinjio ya mifugo ya kisasa ambayo ipo Ndembezi, ina kamilika na kuanza kufanya kazi.

Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu, amempongeza Mbunge Katambi, kwa kufanya kazi kwa vitendo, pamoja na kuitendea haki Wizara ambayo ameteuliwa na Rais Samia.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salu Ndogo, ambaye ni Afisa mipango miji na Mkuu wa idara ya ardhi,  amesema wamejipanga vyema kutatua changamoto zote za wananchi.

Pia amesema kwenye Kata hiyo ya Kolandoto watafika mwezi September kupima ardhi na kurasimisha, hali ambayo itasaidia kutatua migogoro ya ardhi na kuwataka wananchi waendelee kulipia gharama za upimaji wa ardhi zao.

Mbunge Katambi ameanza ziara yake leo Jimboni mwake kwa ajili ya kuzindua miradi ya maendeleo ukiwamo ujenzi wa kisima cha maji Shule ya Sekondari Kolandoto na Daraja la  uzogore- Bugwandege, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, akizunguza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kolandoto.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi na wananchi wa Kolandoto
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Manispaa ya Shinyanga Salu Ndongo, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi, na wananchi wa Kolandoto.
Baadhi ya wananchi wa Kolandoto wakiwa kwenye mkutano wa Mbunge Katambi
Mkuu habari, nilichelewa kutuma Sababu ya Mazingira picha zilikuwa kwenye Camera
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...