
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa akiwa kwenye sehemu maalum akipokea salamu za Bendera katika Sherehe za KMKM DAY zilizofanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa akiwa na kiongozi wa gwaride Luteni. Mary Maico Hafidhi akipita kukagua gwaride lililoandaliwa katika madhimisho ya KMKM DAY.

Kikundi cha gwaride gadi ya wanawake kikipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana kutoa heshima.

Timu ya kuvuta Kamba ya Nyuki (JWTZ) wanaume (kushoto) na timu ya KMKM wakishindana kuvuta kamba ambapo timu ya kmkm imewavuta timu pinzani.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa akiwahutubia katika sherehe za KMKM DAY zilizofanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.Picha na Makame Mshenga KMKM.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...