Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
KAMPUNI ya Kilimanjaro Biochem Limited imezindua kinywaji kipya aina ya pombe kali ya Kiwingu ambapo kinywaji hichi kitazalishwa katika kiwanda chao kilichopo katika kijiji cha Kifaru wilaya ya mwanga mkoa wa Kilimanjaro na kitasambazwa kuanzia Dar es Salaam na Mikoa mingine.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Exaud Kigahe ambaye alikuwa Mgeni rasmi ameipongeza kampuni hiyo kwa uwekezaji wake ambao umegharimu kiasi cha shilling billion 11.5 ambapo umesaidia uchumi kwa kutoa ajira kwa wananchi 200.
"Kampuni hiyo imeajiri zaidi ya watanzania 50 katika ajira isiyo rasmi kutoka kwa wakulima wadogo na wa kati wanaojishughulisha na kilimo cha mtama katika mashamba yaliyopo wilayani mwanga na wilaya za jirani na zaidi ya hapo , kiwanda chao kinachangia kwenye biashara mbalimbali katika Sekta ya uchukuzi ,ujenzi na ujasiriamali".
Hata hivyo Kigahe ameongeza kuwa kupitia Mradi mpya inakadiriwa kuwa mapato yataongezeka kutoka bilioni 24 za kitanzania mpaka Kufika bilioni 50 za kitanzania ndani ya Miaka mitatu ijayo kuambatana na ongezeko la uchangiaji wa pato la taifa kutoka Shilingi bilioni 6 mpaka Kufika bilioni 15 kwa mwaka.
Pia ametoa wito kwa Watanzania na kuziomba taasisi na makampuni kuiga mfano huu wa kuwekeza kwa kujenga viwanda vya kuongeza thamani mazao yetu ili kuongeza tija na kipato kwa wakulima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kampuni ya Kilimanjaro Biochem Mehul Patel amesema wamejipanga vizuri kuhusu ushindani wa vinywaji vingine na wamewekeza takribani bilioni 11.5 kwa ajili ya uwezeshaji na uzalishaji wa bidhaa.
"Soko la vinywaji nchini Lina ushindani mkubwa hivyo tunajali ubora na kuhakikisha viwango katika kila hatua ya utengenezaji wa kinywaji chetu kipya kinachoitwa Kiwingu na katika ubora wetu na tunatumia ethanol yenye viwango vya juu isiyosababisha uchovu baada ya kunywa na yenye kiwango."
Na Mkuu wa usambazaji na Mauzo kutoka Kampuni hiyo Herman Mathias aliongeza kuwa kinywaji cha Kiwingu kinapatikana kwenye chupa ndogo yenye ujazo wa milimita 250 na usambazaji wa Kiwingu utaanza katika Mkoa wa Dar es salaam na Mikoa yote ya kanda ya ziwa.
Naibu Waziri Wa Viwanda na Biashara Exaud Silaoneka
Akizungumza na Waandishi Wahabari jijini Dar es salaam hafla ya Uzinduzi wa kinywaji Cha "Kiwingu" na kuwapongeza Kampuni ya Kilimanjaro Biochem kwa kutoa ajira kwa wananchi 200
Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Exaud Silaoneka akiambatana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kilimanjaro Biochem Mehul Patel wakizundua kinywaji kipya aina ya Kiwingu jijini Dar es salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...