Charles James, Michuzi TV

MBUNGE wa Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi amefanikisha azma yake ya kumaliza changamoto ya Maji katika Shule ya Sekondari Nakaguru iliyopo katika Kata ya Mchombe.

Kunambi amekamilisha ahadi ya kupeleka maji katika Shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha sita ikiwa ni matunda ya ziara yake aliyofanya Februari mwaka huu ambapo wanafunzi wa shule hiyo walimlalamikia changamoto hiyo.

Awali wanafunzi wa shule hiyo walikua wakisafiri umbali wa kilomita moja kufuata maji lakini sasa watachota maji ndani ya eneo la Shule hiyo.

Kunambi pia amefanikisha upatikanaji wa Bomba la maji mserereko kwa wananchi wa kijiji cha Nakaguru katika kata hiyo ya Mchombe.

Katika ziara hiyo pia Kunambi ametembelea Shule mbili moja ikiwa Shule ya Msingi Ngai ambayo amefanikisha kuanza kwa Ujenzi wa Darasa ambapo awali wanafunzi wa darasa la sita walimlalamikia kusoma kwenye darasa la wazi.

"Ni furaha yangu kuona nimekamilisha ahadi yangu kwa Sekondari ya Nakaguru ya kuwaletea Maji hapa lakini pia kufanikisha kuanza kwa Ujenzi wa Darasa hapa Ngai ambapo mwanzo walikua wakisoma kwenye darasa la wazi ambapo wanafunzi waliteseka nyakati za Mvua.

Ziara yangu hii pia nimekagua ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Nakaguru ambayo yameshakamilika pamoja na madawati yake na sasa wanafunzi watasoma bila tabu,"Amesema Kunambi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mchombe, Bathelomeo Swala amemshukuru Mbunge Kunambi kwa kufanikisha ahadi zake hizo ambapo amesema ujenzi wa madarasa hayo vitakua chache kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii.

Nae mmoja wa wanafunzi wa Sekondari ya Nakaguru Imelda John amemshukuru Mbunge Kunambi kwa kuwaletea maji kwani ilikua ni changamoto ya muda mrefu kwao hivyo sasa wana uhakika wa kupata maji safi kwenye Shule yao.

Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi akimtwisha Ndoo ya Maji mmoja wa wananchi wa kitongoji cha Nakaguru B baada ya kufanikisha mradi wa Maji kwenye kitongoji hiko.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi akifungua maji ya Bomba katika Shule ya Sekondari Nakaguru iliyopo Kata ya Mchombe.

Muonekano wa jengo la darasa katika Shule ya Msingi Ngai ambalo Mbunge wa Jimbo la Mlimba Godwin Kunambi amefanikisha ujenzi huo.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi akiambatana na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM na watendaji wa Serikali Halmashauri ya Mlimba wametembelea Shule ya Msingi Nakaguru iliyopo Kata ya Mchombe jimboni hapo na kujionea ujenzi wa madarasa mawili ambayo yamejengwa na Mbunge huyo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...