Makamu wa Rais amekutana na kufanya mazungumzo na shirikisho la wafanya biashara wa Ufaransa ( MEDEF) Paris – Nchini Ufaransa.
Makamu wa Rais aliwahakikishia
Wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu
Hassan inachukua hatua mbalimbali kuboresha mazingira ya uwekezaji na
ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uchumi wa Tanzania na hivyo uwekezaji
wao utakuwa katika mikono salama.
Makamu wa Rais aliwafahamisha
wafanyabiashara hao baadhi ya jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali ili
kuvutia wawekezaji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kisasa kama Reli
ya Mwendokasi (Standard Gauge Railway), mradi wa umeme wa Julius Nyerere
utakaozalisha megawati 2115, miradi ya maji na uboreshaji wa miundombinu ya
barabara na usafiri wa anga.
Kwa upande wao, Kampuni hizo zilionesha
kuridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha
mazingira ya uwekezaji na kuahidi ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa
miradi ya kipaumbele. Aidha, kama ishara ya kuunga mkono jitihada hizo, Kampuni
hizi zilifahamisha kuwa zinatarajia kufanya ujumbe ziara nchini Tanzania kabla
ya mwisho wa mwaka 2021 ili kuangalia fursa za uwekezaji.
Baadhi ya Kampuni kubwa za Ufaransa
zilizoshiriki mazungumzo hayo ni pamoja na TOTAL ÉNERGIES na AIRBUS ambazo
tayari zimefanya uwekezaji mkubwa nchini katika maeneo mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...