Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MBUNGE
wa viti maalum mkoani Pwani ,Subira Mgalu pamoja na UWT Kibaha Mjini,
amekemea baadhi ya wanasiasa pinzani wanaotoa sauti kinzani kumshinikiza
Rais Samia Suluhu ,kuhusu mabadiliko ya katiba kuwa ,wasijaribu
kumtingisha ,kwani kibiriti kimejaa na njiti zake zinawaka .
Ameeleza
wanawake wa UWT na watanzania wanaolitakia Taifa mema wapo nyuma yake
na hawatakubali kuona anabezwa ,anashinikizwa wala kupewa amri .
Akizungumza
katika kongamano lililoandaliwa na UWT Kibaha Mjini ,kupongeza siku 100
na hotuba aliyoitoa Rais Samia kwa wanawake pale Dodoma ,Juni 8 mwaka
huu, Mgalu alieleza ,Rais apewe nafasi kuendeleza Yale aliyoyaacha Rais
wa awamu ya tano marehemu John Magufuli .
Alitoa rai watu hao wapuuzwe kwa maslahi ya nchi na kuendelea kulinda amani iliyopo.
"Ndio
kwanza Rais amefikisha siku 100 ,badala ya kupongeza aliyoyafanya hadi
sasa ,wapo baadhi ya wanasiasa pinzani wanajitokeza kuanza kushinikiza
masuala ya katiba, ameshasema katiba ina umuhimu wake ,apewe nafasi
kutatua changamoto za watanzania katika sekta mbalimbali "
Hata
hivyo ,alimpongeza Rais Samia, kwa bajeti ya kwanza kupitishwa bungeni
kwa asilimia kubwa,huku akishukuru majimbo kupokea milioni 500 kila
jimbo ambapo Pwani imeshapokea bilioni 4.5 kwa majimbo Tisa.
Pia imetolewa bilioni 100 ili kukamilisha maboma ya vituo vya afya 1,500 nchini na zahanati hatua ambayo inahitaji pongezi.
Alikadhalika
Mgalu alimpongeza Rais kwa hatua ya kutoa maelekezo ya kuunganishwa
umeme kwa 27,000 mjini na vijijini ,Bima ya afya kwa kaya zeenye kipato
kidogo bilioni 149 ,mikopo kwa vijana vyuoni bilioni 570 na kutatua
kero ya madai ya wafanyakazi wastaafu mifuko ya hifadhi ya jamii
serikali inalipa tilioni 8 kwa utaratibu wa kutoa hati fungani isiyokuwa
na cash.
Nae mwenyekiti
wa UWT Kibaha mjini ,Elina Mgonja aliwaomba wanawake wamuunge mkono Rais
Samia kwa kazi kubwa ambayo ameanza kuionyesha ndani ya siku 100 kuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ametaka wanasiasa hao wasimsumbue mama na kusababisha kumuondoa katika reli .
Akielezea
kongamano hilo, Mgonja alisema wamezindua ujenzi wa jengo duka maalum
la kuuzia biashara na darasa la ujasiriamali ili kumkwamua mwanamke
kiuchumi .
Alisema
,maelekezo yaliyotolewa Dodoma kupitia mkutano wa wanawake wao wanafanya
kwa vitendo na kumhakikishia mwenyekiti wa CCM Taifa kuwa wataendelea
kumshika mkono mwanamke wa Kibaha ili kujiinua kimaendeleo.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri ambae alimwakilisha
mkuu wa mkoa wa Pwani ,Aboubakar Kunenge ,Sara alisema vikundi vya
ujasiriamali hufa kutokana na kukosa mshikamano ,amewapongeza wilaya
hiyo kuwa na Umoja na mshikamano.
Alisema
hitaji la watanzania ni kutatuliwa changamoto zao ,kutatua migogoro
mbalimbali ya kijamii ,kiuchumi na sio katiba kwasasa ukizingatia nchi
imetoka kupata msiba mkubwa wa kuondokewa na Rais madarakani ,Hii ni
bado muda mfupi sana kushinikiza mambo ambayo yanahitaji muda .
Makamu
mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Selina Wilson alisema, kwa
kutambua vikundi vya ujasiriamali, halmashauri imetoa milioni 600 ndani
ya miezi sita ikiwa ni asilimia 60 kwa mikopo ya akina mama.
Katika
uzinduzi wa ujenzi wa duka la kibiashara Mgalu amechangia matofali
500,mbunge Silvestry Koka mifuko 50 ya saruji,madiwani viti maalum
mifuko 250 ya saruji na sh.500,000 kutoka kwa mwenyekiti wa halmashauri .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...