Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Khamis Juma
amesema serikali inathamini michango ya wanasayansi katika uibuaji wa
tafiti mbalimbali zenye lengo la kuondoa changamoto zinazokabili taifa.
Alisema
hayo jana wakati akizindua mradi wa kuimarisha mifumo ya sayansi,
teknolojia na ubunifu nchini Tanzania wenye lengo la kwenda sanjari na
maendeleo endelevu ya dunia.
Mradi
huo unafanyika chini ya ushirikiano wa UNESCO, Tume ya Taifa ya UNESCO,
Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar.
Alisema
kutokana na umuhimu wa mradi huo serikali imewataka wadau wote kutoa
ushirikiano wa kutosha kuweka misingi ya utafiti, uendelevu wake na
kusaidia watunga sera kutambua nguvu kubwa ya taifa katika kusaidia
kubadili maisha ya wananchi kupitia tafiti.
Katibu
Mkuu huyo akifafanua zaidi alisema kwamba ni matumaini ya serikali
washiriki watasaidia kuchangia uandishi wa msingi wa ripoti
itakayowezesha uimarishaji wa hatua za kuimarisha sera na ubunifu katika
sayansi na teknolojia.
Aliwataka
wadau kuunga mkono jitihada za serikali na UNESCO za kuimarisha utafiti
wa kisayansi na ubunifu ili kuchangia kiuchumi na kujikinga na majanga
Mkuu
wa Ofisi, UNESCO Dar es Salaam, Dos Santos Tirso katika hotuba yake
ilyosomwa na Mkuu wa kitengo cha Elimu UNESCO, Bi. Faith Shayo alisema
kwamba shirika hilo limefurahishwa kufanyakazi na serikali kuhakikisha
mradi huo unafanikiwa.
Alisema
mradi huo umelenga kusaidia Mataifa Wanachama kutekeleza Pendekezo la
Watafiti wa Sayansi na Teknolojia 2017, kwa nchi sita za Afrika tangu
Septemba 2020 za Ghana & Sierra Leone,Tanzania, Namibia, Zimbambwe
na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mradi
utatekelezwa kwa awamu mbili na awamu ya majaribio ya: Septemba 2020
-Agosti 2022 na Awamu ya II: Septemba 2022- Agosti 2025. Bajeti
iliyotengwa kwa awamu ya majaribio ya mradi nchini Tanzania ni Dola za
Marekani 250,000.
Awali
akitambulisha mradi huo Mkuu wa kitengo cha Sayansi asilia na Mratibu
wa mradi huo kutoka UNESCO, Bw. Keven Robert alisema kuwa mradi huo
utawezesha kusaidia nchi kuimarisha mifumo ya sayansi, teknolojia na
utafiti.
Aidha
mradi huo pia utasaidia kuimarisha taasisi za kisayansi kufanya tafiti
na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya tafiti za kisayansi ambazo
zitasaidia katika kutatua changamoto za wananchi, kukabiliana na majanga
yakiwemo magonjwa mbalimbali na pia kufikia malengo ya maendeleo
endelevu.
Robert
alisema kuwa mradi huo utakuwa na maeneo10 ya utekelezaji ambapo baadhi
ya maeneo ni pamoja na kuangalia uwekezaji katika tafiti za kisayansi
ambapo matokeo ya tafiti hizo zinapouzwa zinaweza kuimarisha uchumi ya
nchi.
“Mfano
katika kipindi hiki cha janga la Corona yapo mataifa yaliyofanya tafiti
za kisayansi na kutengeneza chanjo hivyo zinapouzwa mataifa hayo
yamekuwa yakipata fedha na kukua kiuchumi,” alisema Robert.
Alitaja
maeneo mengine yatakayoangaliwa katika mradi huo kuwa ni kwa namna gani
tafiti za kisanyansi zinasaidia wananchi na kwa namna gani wananchi
wanashirikishwa kwenye tafiti kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani
Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi
wa mradi wa kuboresha mifumo ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kwa
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya
UNESCO katika hafla fupi iliyofanyika kwenye hoteli ya Madinat Al Bahir
visiwani Zanzibar. Kulia ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya
Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel na kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi
Mkazi wa UNESCO, Bi Faith Shayo.

Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Bi Faith Shayo akitoa neno la ukaribisho
kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuboresha mifumo ya
Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO katika hafla fupi
iliyofanyika kwenye hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar.

Mwakilishi
wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel akitoa
salamu za NATCOM wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuboresha mifumo ya
Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO katika hafla fupi
iliyofanyika kwenye hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar.


Mkuu
wa kitengo cha Sayansi asilia na Mratibu wa mradi huo kutoka UNESCO
Keven Robert akitoa muhtasari wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji
wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu (STI) kwa ajili ya
Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani kwa ufadhili
wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya
UNESCO katika hafla fupi iliyofanyika kwenye hoteli ya Madinat Al Bahir
visiwani Zanzibar.

Meza
kuu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Bi
Faith Shayo, Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali visiwani Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma pamoja na Mwakilishi wa
Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel wakati wa
uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na
ubunifu (STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania
bara na visiwani kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA)
kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar
pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO katika hafla fupi iliyofanyika kwenye
hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar.


Mgeni
rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani
Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma (katikati) akikata utepe kama ishara ya
kuzindua mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na
ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara
na visiwani kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa
ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bara na
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya
Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani
Zanzibar Wanashiriki tukio hilo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa
UNESCO ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Elimu wa shirika hilo nchini,
Bi.Faith Shayo (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume
ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).

Mgeni
rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani
Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma (wa tatu kulia) akimkabidhi Naibu Makamu
Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri Elekezi wa Chuo Kikuu cha Taifa
Zanzibar (SUZA), Dr Ali Ussi nakala ya mradi wa uimarishaji wa mifumo ya
Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia bara na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika
hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar Wanaoshuhudia tukio hilo ni
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO ambaye pia ni Mkuu wa kitengo
cha Elimu wa shirika hilo nchini, Bi.Faith Shayo (kushoto) pamoja na
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel
(kulia).

Mgeni
rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani
Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma (wa tatu kulia) akimkabidhi Mjumbe wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Yahya Abdulla nakala ya mradi wa
uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili
ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani kwa
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na
UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bara na Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM)
uliofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar
Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO
ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Elimu wa shirika hilo nchini, Bi.Faith
Shayo (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya
Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).

Mgeni
rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani
Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Elimu wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bw. Omar Ali nakala ya mradi wa uimarishaji
wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani kwa ufadhili wa Shirika
la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia bara na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika
hoteli ya Madinat Al Bahir visiwani Zanzibar Wanaoshuhudia tukio hilo ni
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO ambaye pia ni Mkuu wa kitengo
cha Elimu wa shirika hilo nchini, Bi.Faith Shayo (kushoto) pamoja na
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel
(kulia).


Baadhi
ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali za sekta binafsi, serikali,
waandishi wa habari pamoja na jamii walioshiriki uzinduzi wa mradi wa
uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili
ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania bara na visiwani
unaoratibiwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi
(SIDA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bara
na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa
ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahir
visiwani Zanzibar.
Picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...