ANAONDOKA? Ni swali ambalo mashabiki wa Klabu ya Soka ya Simba huwenda wakajiuliza juu ya mustakabali wa Msemaji wao, Haji Manara kutokana na 'post' yake aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Kupitia ukurasa wake huo, Manara ameeleza kusikitishwa na vitimbi anavyofanyiwa kila siku na baadhi ya watu ambao hajawataja majina ndani ya Mabingwa hao mara nne mfulululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
" Hivi vitimbi mnavyonifanyia kila siku kisa Simba vishanichosh
a, mwisho wa siku mtanitoa roho yangu kabla ya muda wangu, Imetosha kwa sasa!!
Ubaya wote ni Haji lakini mafanikio ni yenu nyie wakubwa, kila siku ni Haji Haji Haji," Ameandika Manara.
Ameendelea kwa kuandika kuwa, " Mkitoka kunisingizia hili mtatengeneza sinema nyingine kwangu, tunashindwa kujua kila mja Mungu amempa fungu lake, inakuaje riziki ya umaarufu wa mwenzio iwahangaishe kiasi hicho? Likitokea baya pakuanziq mnapo,"
Bado haijafahamika ni watu gani ndani ya Simba ambao wanamuonea wivu lakini ni dhahiri kuwa Kuna fukuto ndani ya Klabu hiyo ikiwa zimebaki siku kadhaa kumenyana na watani wao Yanga katika fainali ya Kombe la FA Mkoani Kigoma Jumapili ya Julai 25.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...