Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA -Kihonda mkoani Morogoro( kushoto) akiwa katika banda la VETA lililopo maonesho ya biashara ya kimataifa ,Dar es Salaam.

Wananchi waliotembelea banda la VETA wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa watalaamu wa Chuo cha Veta Kihonda.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MWANAFUNZI wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Ufundi VETA Kihonda mkoani Morogoro Nyerere Kalage amesema iwapo atakutana na Rais Samia Suluhu Hassan atamuelezea namna ambavyo amefurahishwa na hatua ya Serikali yake kuona na kutambua thamani ya vijana wa Tanzania kwa kuhakikisha wanakwenda kupata mafunzo ya miezi sita kwenye vyuo vya VETA kama sehemu ya kuwajengea uwezo.

Akizungumza kwenye Banda la VETA lililopo katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Dar es Salaam, Kalage amesema iwapo atamwambia aendelee kuweka juhudi kwa vijana kama alivyoamua kusomesha vijana bure VETA  ile kozi ya miezi sita, kwani hiyo yote inaonesha anathamini vijana wa nchi hii.

"Imekuwa ni fursa na watanzania wengi wamechangia kozi za VETA ambazo Serikali imeamua kutoa mafunzo bure lakini waliojitokeza ni wengi kuliko ambao wamepata lakini ni matumaini yangu Serikali itaangalia namna bora zaidi ya kuhakikisha vijana wengi wanapata nafasi hiyo ambayo Rais ameamua kuitoa kwa ajili yetu vijana,"amesema.

Akizungumzia Maonesho hayo na uwepo wa Banda la VETA, amesema yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho cha VETA Kihonda lakini ameona fursa nyingi na hasa ubunifu ambao umefanywa na watanzania kutoka mikoa mbalimbali nchini walioko chini ya VETA.

"Nikiwa kama mwanafunzi na katika maonesho haya tumekuja na mashine ambazo zimebuniwa na wanafunzi na nyingine zimebuniwa na walimu ambazo zinatumika kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo.Tunayo mashine ya kusaga karanga ili kupata siagi ya karanga iliyo bora na inayoweza kuuza sehemu yoyote na ikapata soko.

"Tuliamua kuongeza thamani ya zao la karanga baada ya tafiti na kubaini wamama wengi wamejiajiri katika bishara ya siagi lakini changamoto kubwa waliyonayo ni kukosa mashine ambazo zinaweza kutumika kusaga karanga katika ubora unaotakiwa,"amesema.

Amesema hivyo kwa kutumia mashine hizo ambazo zimebuniwa na wanafunz na walimuwa VETA Kihonda zinakwenda kutatua changamoto hiyo ambayo imekuwa ikisababisha wanaojihusisha na biashara ya kuuza siagi ya karanga kukosa soko kwa kuwa na siagi ambayo haiko kwenye ubora."Wanaohitaji mashine hizi waje Chuo cha VETA Kihonda au wanaweza kwenda chuo chochote cha VETA nchini itakuwa rahisi kuipata."

Aidha ametoa pongezi kwa uongozi wa VETA kwa kuhakikisha inawakutanisha wabunifu kutoka mikoa mbalimbali nchini kwani imekuwa sehemu ya wao wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kuona kazi za wengine ambavyo zimefanyika na matarajio yake mwakani naye atakuwa katika maonesho hayo na kitu ambacho atakuwa amekubuni mwenyewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...