Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula akimjulia hali Mzee Mohamed Kidume mkazi wa Mtwara
Mikindani mwenye umri wa miaka 97 katika eneo la Mji wa Kale wakati wa
ziara yake mkoani Mtwara. Mzee Kidume ni mmoja wa wazee waliompokea Mwl.
Nyerere wakati wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akizungumza na wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa
Mtwara tarehe 23 Julai 2021 wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa
sekta ya ardhi mkoani humo.Sehemu ya Wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mtwara
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya
ardhi katika mkoa wa Mtwara tarehe 23 Julai 2021.
Mmoja
wa wananchi wa Mtwara Sheikh Nurdin Abdalaah Manguji anayemiliki
takriban hekta 8.704 katika eneo la Shangani West Mtwara aliimuomba
serikali kupitia wizara ya Ardhi kumsamehe kodi anayodaiwa miaka ya
nyuma kwa kuwa hakuwahi kufahamishwa na kupatiwa nyaraka za eneo lake.
mkazi wa Mtwara Sheikh Nurdin Abdalah Manguji akiwasilisha kero yake ya ardhi kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani humo.
Na Munir Shemweta, MTWARA
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
amewataka watendaji wa sekta ya ardhi kushiriki katika ziara za viongozi
ili kuweza kujibu changamoto zitakazojitokeza wakati wa ziara.
"Kiongozi
akija eneo lako hakikisha uko katika msafara kama suala la ardhi
likijotokeza basi wewe uweze kutoa ufafanuzi ili hatua zichukuliwe"
alisema Dkt Mabula
Akizungumza
na watendaji wa sekta ya ardhi mkoani Mtwara tarehe 23 Julai 2021, Dkt
Mabula aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi katika mikoa kuhakikisha
wanakuwa na daftari maalum la kuorodhesha migogoro ya ardhi na hatua
zilizochukuliwa sambamba na kuandika taarifa kuhusiana na migogoro
husika kwenda ofisi za wakuu wa wilaya.
"Kumekuwa
na utaratibu akija kiongozi mpya migogoro inaibuka upya sasa mhakikishe
migogoro hiyo inaandikwa kwenye mfumo wa matrix ili kmrahisishia
kiongozi na kumuepusha kupokea malalamiko yaliyokwisha fanyiwa kazi.
Aidha,
katika kuhamasisha wanachi kulipa kodi ya ardhi Dkt Mabula alizitaka
halmashauri kuandika taarifa ya jinsi zilivyotoa elimu kwa umma kupitia
vyombo vya habari kama vile redio za kijamii.
Pia
aliwaeleza watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Mtwara kuwa
anafikiria namna ya kuanzisha ushindani wa ukusanyaji kodi ya ardhi
katika halmashauri kwa lengo la kuona halmashauri iliyofanya vizuri
zaidi.
katika kujenga
nidhamu ya watumishi, Dkt Mabula aliagiza watumishi wa sekta ya ardhi
kutotoka nje ya vituo vyao vya kazi bila wakurugenzi kuwa na taarifa na
kusisitiza kuwa watumishi wa ardhi wanatakiwa kutatua migogoro na si
kuwa sehemu ya migogoro.
Akielezea
upangaji miji katika maeneo mbalimbali nchini Naibu Waziri wa Ardhi
alisema, pamoja na Wizara kusaidia harakati za upangaji Upimaji na
umilikishaji ardhi katika halmashauri lakini jukumu la upangaji linabaki
kwa halmashauri kwa kuwa ndiyo mamlaka ya upangaji.
"
Si jukumu la wizara kuingilia upangaji wa miji katika halmashauri ila
inazisaidia kuzikopesha fedha na kueleza kuwa zipo halmashauri
zilizopewa milioni 200 hadi 300 lakini zipo nyingine zimetumia fedha kwa
mambo mengine na nasisitiza pesa ziende katika masuala ya ardhi"
alisema Dkt Mabula.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...