Bahati Habibu Maelezo Zanzibar. 16/7/2021.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini, Khamis Hamza Chilo, amewataka madaktari na wahudumu wa Afya kutoa huduma zilizobora licha ya mazingira magumu wanayokutana nayo.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada wa vifaa kwa ajili ya vituo mbalimbali vya afya, huko Mwera Wilaya ya kati Unguja, Mbunge huyo alisema Jimbo la Uzini bado linahitaji mikakati madhubuti ili wananchi wa jimbo hilo waweze kupata huduma bora za afya.

Amesema madaktari na wahudumu wa Afya bado wanakabiliwa na changamoto, ikiwemo uhaba wa vifaa, na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na Serekali, wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa jimbo hilo.

“Kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi na Viongozi wa Jimbo la Uzini kwa kushirikiana na Serikali tutazitatua changamoto hizi kila hali itakaporuhusu”. alisema Mbunge huyo

Alieleza kuwa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inaendelea na jitihada za kuhakikisha wananchi wote wa Zanzibar wanapatiwa huduma bora za afya Nchini, hivyo aliwataka wahudumu wa afya kufanya kazi kwa bidii.

Amesema msaada huo wa Magodoro na mito wenye thamani ya shilingi 2,275,000/= utatumika katika vituo vya afya ambavyo vinahudumia wazazi, akinamama na watoto.

Nae Mwakilishi wa Jimbo hilo Haji Shabani Waziri amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya maradhi ya Corona ambayo tayari Wizara ya Afya ya Zanzibar imethibitisha kuwepo kwa wagonjwa wa Corona Zanzibar.

Aidha amewataka madaktari kutumia taaluma yao katika kutoa elimu kwa Jamii ili kujikinga na maambukizi ya corona, ikiwa ni pamoja na kuvaa Barakoa ,kunawa mikono kwa maji na sabuni na vitakasa mikono na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

Nae Afisa tabibu wa kituo cha afya Mwera, Dokta Salum Makame ameushukuru uongozi wa Jimbo la Uzini kwa Juhudi wanazozichukua za kuimarisha sekta ya afya katika Jimbo hilo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...