Wakati mashindano ya michezo mbalimbali ya majeshi yanatarajiwa kuanza Agosti 4 mwaka huu jijini Dodoma, benki ya NBC limetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ili kusapoti jitihada za jeshi hilo katika sekta michezo.


Vifaa hivyo zikiwamo viatu vya michezo, mipira, jezi pamoja na vifaa vingine vya michezo mbalimbali vilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa michezo Kanda ya Ngome, Kanali David Mziray, na Meneja wa NBC tawi la Dodoma, Bi Happiness Kizigira.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo, Kanali Mziray alisema vitasaidia kuongeza hamasa kwa wachezaji wa timu za JWTZ ambao wamepania kuchukua vikombe mbalimbali vya mashindano hayo.


“Kupata kwa vifaa hivi kutawasaidia wachezaji wetu kuongeza hamasa zaidi kwenye mashindano hayo ambayo timu zetu zimepania kunyakua makombe yote,” alisema Mziray.


Meneja wa NBC tawi la Dodoma Bi Happiness Kizigira akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo, alisema wametoa vifaa hivyo kutokana na kuwapo na Ushirikiano kati ya benki hiyo na jeshi la wananchi.


“Benki ya NBC tumekuwa na mahusiano mazuri ya muda mrefu na Jeshi la Wananchi na kwa kuwa mwezi ujao wenzetu watakuwa na jambo lao hapa Dodoma ambalo kimsingi tunawaombea mafanikio sana tumeona ni vema tuwaunge mkono ili mambo yaende vizuri zaidi,’’ alisema Kizigira.


Kizigira alisema vifaa hivyo wamevitoa Makao Makuu ya Jeshi kwa lengo la kuweza kuwafikia wanamichezo wote wa jeshi hilo ambao watashiriki mashindano hayo mwaka huu.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Wateja Binafsi Benki ya NBC, Bw Abel Kaseko (Kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa michezo Kanda ya Ngome, Kanali David Mziray ikiwa ni msaada wa benki hiyo kwenda kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya michezo mbalimbali ya majeshi yanayotarajiwa kuanza Agosti 4 mwaka huu jijini Dodoma. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni maofisa wa benki hiyo pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Wateja Binafsi Benki ya NBC, Bw Abel Kaseko (Kulia) na Mwenyekiti wa michezo Kanda ya Ngome, Kanali David Mziray wakikata utepe kuashiria mahusiano mema baina ya taasisi hizo mbili.
Meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Bi Happiness Kizigira (Kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo kwa mmoja wa maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya michezo mbalimbali ya majeshi yanayotarajiwa kuanza Agosti 4 mwaka huu jijini Dodoma.
Maofisa wa benki ya NBC pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...