Na Amiri Kilagalila,Njombe
CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe kimetaka wananchi kuendelea kuchukua
tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID 19 kwa kuzingatia usafi,kuvaa
barakoa ,utumia vipukusi na kuepuka mikusanyiko.
Akizungumza
na wandishi wa habari katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto
Ngole amesema Corona ipo nchini kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania alivyoagiza hivyo kila mwananchi achukue tahadhari.
"Rais
ametuelekeza juu ya ugonjwa wa Corona,lazima niwaambie ndugu zangu hata
Njombe kuna Corona na serikali imekuwa wazi tuchukueni
tahadhari"alisema Erasto Ngole
Aidha
bwana Ngole akizungumzia swala la katiba pya amesema siyo kipaumbele
cha serikali ya awali ya sita ambapo juhudi zinazofanyika ni kutatua
changamoto zinazowakabili Watanzania kwa kusimamia miradi ili Ilani
itekelezwa kikamilifu.
"Katiba
mpya sio kipaumbele cha watanzania kwa sasa wala sio kipaumbele cha
serikali ya awamu hii.Kipaumbele ni kutatua changamoto zinazowakabili
wananchi,tumejikita kutekeleza Ilani ya CCM ambayo ndio deni letu kwa
wananchi,katiba mpya itakuja baada ya kupunguza mzigo wa changamoto
unaowakabili watanzania"alisema Ngole
Nae
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Isaya Mwasubila amesema
serikali kupitia watalaamu wa afya wanaendelea kutoa elimu ya kujikinga
na CORONA huku akiagiza maeneo ya ofisini na kwenye mikusanyiko
kuhakikisha wanaweka ndoo za maji ya kunawa,kuvaa barakoa na kupaka
vipukusi mikononi.
"Ni
tahadhari ambazo zinaendelea kuchukuliwa ikiwemo na zile za awamu ya
kwanza,pia kwenye awamu hii ya tatu hatua ni zile zile ikiwemo kunawa
mikono kwa maji safi na tiririka pia kuepuka misongamano"Alisema Isaya
Mwasubila
Baadhi ya
wananchi waliozungumza na kituo hiki wamesema serikali kupitia watalaamu
inatakiwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujikinga na Corona
kwa kuwa bado kumekuwa na hali ya upuuziaji kati jamii dhidi ya
kujikinga na Corona.
Vile
vile Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe kimempongeza kwa dhati
Rais Samia kwa kupokea kijiti katika mazingira magumu baada ya aliyekuwa
Rais wa Tanzania Mh, John Pombe Magufuli kufariki dunia huku nchi
ikiendelea kutulia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...