Na Amiri Kilagalila,Njombe
Watoto
wawili wakike na wakiume (mapacha) wenye umri wa miaka 9 na wakiume
mmoja mwenye umri wa miaka 11 wametekelekezwa na baba yao mzazi katika
nyumba wanayoishi.
Taarifa
zinaeleza kuwa, baba wa watoto mapacha anayefahamika kwa jina la Edward
Chaula amewatelekeza watoto hao kwa kuondoka na kuikataza jamii kuto
kutoa msaada wowote kwa watoto hao.
Aidha
jamii ilibaini kuwa watoto hao wametelekezwa baada ya watoto hao
kuonekana wakizagaa mitaani wakiiba kuku ili wafanye kitoweo na kuacha
kuhudhuria shuleni ndipo balozi msaidizi katika mtaa wa mpechi
kuwachukua na kuwafikisha ofisi ya mtendaji ili kupata kibali cha
kuwapeleka wilayani Ludewa aliko mama wa watoto hao.
Chanzo
cha kutelekezwa kwa watoto hao kinatajwa kuwa ni migogoro iliyopo kati
ya wazazi wao ambapo baba anatajwa kuwa amekuwa akimtishia usalama mama
yao ajulikanaye kwa jina la Andowise Mtega endapo atafika maeneo ambayo
wanaishi watoto hao.
Tukio
hili limebainishwa na mwenyekiti wa mtaa wa mpechi kata ya Mjimwema
mjini Njombe Onesmo Kilasi wakati wa mahojiano yake na kituo cha radio
cha Kings Fm baada ya kupata taarifa za tukio kutoka kwa rai wema.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...