Na. Shukrani Kawogo, Njombe.

Wakati serikali wilayani Ludewa ikiendelea kuhamasisha wananchi kulima mazao mbalimbali ya kimkakati kama korosho, parachichi pamoja na kahawa ili kuweza kukua kiuchumi na kujiongezea kipato, wananchi wa tarafa ya masasi wilayani humo wamelalamikia ugumu wa upatikanaji wa pembejeo za zao la korosho ambao hupelekea zao hilo kutohudumiwa  kwa wakati.

 Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga alipotembelea  vijiji vya Kingole, Lifua, Liughai, Kiyogo, Lihagule na Luilo ambako kote alikutana na changamoto hiyo ambayo wananchi wameilalamikia.

Paulo Mbawala ni wakazi wa kijiji cha Luilo amesema kuwa pembembejeo hizo wamekuwa wanazitafuta nje ya wilaya yao kitu ambacho kinawapotezea muda wa kuhudumia zao hilo huku Evelina Haule wa kijiji cha Kingole akisema kuwa kwa sasa korosho hizo zimekuwa na ugonjwa wa "bright" ambao hukausha majani na kuyapukutisha kitu ambacho hupelekea kukosa mazao kwa wingi.

Naye amesema kuwa licha ya pembejeo hizo kupatikana kwa ugumu pia kuna tatizo la soko la zao hilo kwani kwa sasa mazao yao wanaenda kuuzia kwenye mnada unaofanyika wilayani Tunduru kitu ambacho kinawasababishia hasara hivyo wanaomba kusogezewa soko la zao hilo angalau liwekwe Songea.

Ameongeza kuwa endapo soko hilo litasogezwa itakuwa msaada mkubwa sana kwao pamoja na majirani zao ambao ni songea na wilaya ya Nyasa kwani wamekuwa wakilipia tozo ya usafirishaji kiasi cha shilingi 380 kitu ambacho fedha hiyo ingeweze kubaki kuwa faida ya mkulima.

Naye mwenyekiti wa chama cha ushirika wa za hilo wa kata ya Luilo John Ngatunga amesema kuwa sambamba na changamoto hizo pia wanakabili na changamoto ya viatilifu kwani walivyopewa ni vichache kulingana na mwamko wa wakulima waliojitokeza kulima zao hilo.

Mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga amesema suala hilo tayari alishaanza kulifanyia kazi ambapo alishiriki mkutano wa wabunge ambao majimboni kwao wanalima zao hilo lakini inaonekana kuwa katika wilaya ya Ludewa zao hilo hulimwa kwa uchache.

"Wilaya yetu imeonekana zao hili linazalishwa kwa uchache ambapo mwaka juzi tulizalisha tani 101 na mwaka jana tumezalisha tani 64 tu! hivyo ni kiwango kidogo sana kinachopelekea kushindikana kuletwa kwa mnada wilayani kwetu", alisema Kamonga.

Ameongeza kuwa ili kuweza kuimarisha zao hilo atakaa na chama cha ushirika ili waweze kujadili kwa pamoja kwa jinsi gani wanaweza kutatua changamoto hizo za kilimo cha korosho.

Bakari Mfaume ni katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa amewataka wananchi hao kuwa na mwamko katika kulima zao hilo huku akifananisha zao hilo na dhahabu nyeupe.

"Ndugu zangu kama mmeshindwa kwenda kuchimba dhahabu basi dhahabu nyingine inapatikana kwenye miti ya mikorosho tena ni dhahabu nyeupe kabisa! hivyo limeni kwa wingi ili muweze kukuza zao hili na muweze kunufaika zaidi", Alisema Mfaume.

Kwa upande wa afisa kilimo wa wilaya  Amesema katika msimu huu wa kilimo wameweza kuwasaidia wananchi pembejeo za kilimo bure japo hazikuweza kuwafikia wananchi wengi kutokana na kutokuja kwa wingi.

Ameongeza kuwa huo si mwisho bali watakuwa na mgao wa awamu ya pili ambapo wataleta kwaajili ya kuboresha zao hilo huku wakiwaandalia miche laki moja itakayogawiwa kwa wananchi watakaojiorodhesha kulingana na uhitaji wao.

Majani ya mti wa mkorosho ambayo yamepatwa na ugonjwa wa kunyauka majani na kuanza kupukutika ujulikanao kama "bright"
Viongozi wa CCM ngazi ya wilaya wakiwa sambamba na mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga(kushoto) baada ya kuwasili katika kijiji cha Lifua kusikiliza kero za wananchi. Wapili kushoto ni mwenyekiti wa wa chama hicho Stanley Kolimba na anayemfuata ni katibu wa chama hicho Bakari Mfaume.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga, akiongea na wananchi wa kijiji cha Lifua alipofanya mkutano wa kusikiliza changamoto mbalimbali.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (aliye simama) akiwapigia makofi watumbuizaji wa ngoma ya mahalamisi.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa ameungana na wacheza ngoma ya mganda iliyokuwa ikitumbuiza katika mkutona katika kijiji cha Luilo.
Wakanakikundi cha ngoma kijulikanacho kama mahamisi kutoka kijiji cha Lifua, wakimpa zawadi ya mpunga mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kwa kumtwisha kichwani.
Moja ya shamba la korosho lililopo katika tarafa ya masasi wilayani Ludewa
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...