KAMPUNI ya simu Infinix yatanguliza shukrani zake kwa mapokeo mazuri ya promosheni ya Infinix NOTE 10 ambapo jumamosi hii ndio hitimisho la promosheni hii. Infinix itakita kambi katika maduka ya simu kariakoo kwa siku nzima ambapo Infinix itafanya punguzo la bei kwa simu za Infinix NOTE 10 na NOTE 10 pro pamoja na zawadi ya blenda, jagi la umeme kutolewa papo hapo kwa wateja wa NOTE 10 na baadhi ya zawadi kama music system zitatolewa kwa mfumo wa bahati nasibu.
lakini pia kwa siku hiyo Infinix NOTE 10 itapatikana kwa bei punguzo badala ya kulipia 530,000Tsh utaipata kwa sh. 430,000 na NOTE 10 pro utaipata kwa sh.550,000 badala ya kulipia sh.700,000. Afisa Mahusiano Infinix, Aisha Karupa amesema, “katika simu ya mwisho ya promosheni ya NOTE 10 Big mnyama tumeamua kufanya punguzo kubwa ili kila mwenye Nia basi huu ni wakati sahihi wakuimiliki simu hiyo ambayo inafanya vizuri sokoni kutokana na uwezo wa kumudu application zenye ujazo mkubwa.”
Infinix NOTE 10 na NOTE 10 pro zilizinduliwa mapema mwezi May nchini Tanzania na sifa kuu ya simu hizi ni ufanisi wa G95 processor na kamera ya MP64 na teknolojia ya 4K video resolution ambayo ndio teknolojia bora kwa sasa katika kutengeneza filamu.

Kwa punguzo na zawadi mbalimbali kutoka Infinix bila ya kukosa tembelea maduka ya simu kariakoo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...