Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeibuka kidedea kwa kuwa Mshindi wa pili kwenye kundi la Wadhibiti kwenye Maonesho ya Sabasaba mwaka 2021.
Akizungumza baada ya ushindi huo Mkuu wa kitengo Cha Masoko na Uhusiano kwa Umma, Shamim Mdee amesema PSPTB imekuja kivingine mwaka huu kwa kuja na Ubunifu mpya katika masuala ya Ununuzi na Ugavi ndio maana imeshika nafasi nzuri katika Tuzo hizo za Maonesho ya mwaka huu.
Mdee amesema Ushindi huo umepatika baada ya kukidhi vigezo mbalimbali vya ushindi ikiwemo ubora wa banda (branding), Ubunifu, Huduma bora kwa wateja na utoaji bora wa Elimu.
Katika kundi hilo mshindi wa kwanza amekuwa Benki ya Tanzania (BOT) na mshindi wa tatu Mamlaka ya Udhibiti ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...