Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge, amesema hatosita kumchukulia hatua
kali ya kisheria yeyote yule atakaefanya uvamizi wa ardhi wa aina
yeyote.
Alieleza hayo
wakati wa kuzindua Kampeni ya kushughulikia Migogoro ya Sekta ya Ardhi
Mkoani Pwani,uzinduzi uliofanyika Mjini Kibaha,uliomshirikisha William
Lukuvi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi wa Halmashauri na Kamati ya Usalama ya Mkoa.
Alieleza
kuwa watafanya ziara na Waziri wa Ardhi katika Wilaya za Kibaha,
Bagamoyo, Mafia, Mkuranga, Rufiji na Kibiti kuanzia Tarehe 14
Julai,2021 hadi Tarehe 22 Julai 2021 kushughulikia na kutatua Migogoro
ya Ardhi.
Kunenge,
aliwataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote Mkoa wa Pwani kuhakikisha
wanatumia nafasi zao katika kutatua migogoro ya Ardhi.
Kunenge
pia aliwataka Viongozi hao wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaboresha
Daftari la makazi na kuhakiki idadi ya mifungo iliyopo mkoani Pwani ili
kuepukana na Migogoro ya Ardhi.
Naye
Waziri Wa Ardhi Lukuvi kwa Upande wake amewataka Wakuu wa Wilaya
kuhakikisha wanatatua migogoro ya Ardhi na wasisubiri mpaka wananchi
waje kulalamika kwa Viongozi wakuu,
Aliziagiza
Halmashauri zote Tanzania kuhakikisha wanazisimamia kampuni binafsi za
upimaji wa ardhi na wasiziache zikafanya kazi zenyewe.
“Kampuni
Binafsi lazima zisimamiwe na zisiachwe zifanye kazi zenyewe kwani
msimamizi wa Ardhi katika Halmashauri ni Halmashauri” alisema Lukuvi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...