Msanii Wa Bongofleva Hamorapa akiingia katika ukumbi wa Samaki Samaki Mlimani city wakati wa hafla hiyo ya kutambulisha 18 Bora waliochaguliwa kuingia kambini.
Washiriki 18 wa Shindano la Bingwa lililoandaliwa na Kampuni ya Startimes wakikabidhiwa zawadi ya ving'amuzi kwa ajili ya wapendwa wao Nyumbani kuwatazama katika chaneli mpya ya Tv3 pindi watakapoingia mjengoni.

Na Khadija Seif, Michuzi Tv

WASHIRIKI 18 Watinga  Msimu wa Kwanza wa Shindano la Bingwa kitakachorushwa kupitia Tv3 katika King'amuzi cha Startimes.

Shindano hilo la Bingwa ambalo lilifunguliwa siku za karibuni na kukutanisha watu maarufu mbalimbali wenye ushawishi katika jamii ambao walipendekezwa katika ukurasa wa Mtandao wa kijamii wa Instagram nakutakiwa mashabiki wao kuwapigia kura za kutosha ili kuwawezesha Washiriki 16 kuingia katika jumba la Bingwa rasmi.

Akizungumza na Waandishi Wahabari jijini Dar es salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malisa, amesema awali walikua Washiriki 23 ambao waliweza kupendekezwa na hatimaye kuingia kwenye mchakato wa kupigiwa kura za kutosha ili waweze kuingia kambini rasmi.

"Kupitia chaneli ya Tv3 kwenye King'amuzi cha Startimes tumeweza kushirikiana kwa pamoja na kuona kwa jinsi gani washiriki 18 walipigiwa kura kwa haki na ndio hatimaye tumewapata na wataingia kambini kwa ajili ya kuzipigania Milioni 10 pamoja na gari ambalo kwa sasa hatuliweki bayana."amesema.

Aidha, Malisa ameongeza kuwa Reality show hiyo itatazamwa na watu kuanzia umri wa miaka 15 kutokana na kuwepo vitu vingi kuanzia Burudani na Elimu.    

"Zawadi kwa mshindi atakaepatikana kwenye Shindano la Bingwa atajishindia kitita cha fedha taslim milioni 10 pamoja na gari huku washiriki wengine kupewa kifuta jasho." amesema

Pia washiriki hao walioingia kambini watalala kwa muda wa siku 60 bila simu za mkononi na watajifunza vingi wawapo kambini hapo.

Kwa upande wake msanii was vichekesho, Idris Sultan, amesema yeye kama mwongozaji wa shindano hill anaamini watampata Bingwa bora kwa sababu ni washiriki ni watu wenye ushawishi.

"Watakaa kwenye jumba la Bingwa kwa miezi miwili wakiwa hawana simu wala mawasiliano na watu wa nje na kila wiki watakuwa wakitoka washiriki watano hadi atakapo patikana mshindi" amesema Idris.

Kwa niaba ya washiriki msanii Harmorapa amesema amejipanga kuwa mshindi wa shindano hilo na anatarajia kwa kuwa hadi sasa hajaona mshindani wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...