RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa baraka zake na kuunga mkono mashirikiano yanayoimarishwa kati ya Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika suala zima la kuimarisha uwekezaji nchini.
Rais Dk. Mwinyi ametoa baraka hizo katika mazungumzo aliyoyafanya kati yake na uongozi wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) chini ya Mkurugenzi wake Mtendaji Shariff Ali Shariff pamoja na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) chini ya Mkurugenzi wake Mtendaji Dk. Maduhu Isaac Kazi, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Zanzibar.
Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa jambo wanalolifanya na kuendeleza utaratibu wa kukuza mashirikiano ni jambo la busara na lina tija kubwa katika masuala ya uwekezaji hapa nchini kwani fursa zilizopo zinafaa kufanywa kwa pamoja.
Hivyo, alisema kuwa uwamuzi huo anauunga mkono na kuzitakia maendeleo makubwa Taasisi hizo kwa azma ya kufikia lengo lililokusudiwa.
Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa ipo haja ya kuuimarishwa zaidi utaratibu wa Hati ya Maelewano (MOU) iliyokuwepo hapo awali kwani wakati umefika kwa yale yaliyokuwa hayamo yaweze kuigizwa kwenye (MOU) hiyo kwa lengo la kupata tija zaidi kwa pande zote mbili.
Alisema kuwa suala la kubadilishana uzoefu kati ya Taasisi mbili hizo ni jambo muhimu sana hatua ambayo itasaidia kupatikana kwa mafunzo kwa watendaji wa Taasisi hizo kwa azma ya kuimarisha sekta ya uwekezaji hapa nchini.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi alieleza ndoto yake ya kuona kwamba Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) inakuwa na Kituo Kimoja cha Kutoa Huduma.
Aliongeza kuwa hatua hiyo ya kuwa na Kituo Kimoja cha Kutoa Huduma itasaidia kuondosha urasimu na ucheweleshaji wa kutoa huduma kwa wawekezaji na kuifanya sekta ya uwekezaji kuwa rahisi hapa nchini.
Home
BIASHARA
RAIS WA ZANZIBAR DKT MWINYI AZIUNGA MKONO USHIRIKIANO MAMLAKA ZA KUKUZA UWEKEZAJI ZANZIBAR (ZIPA) NA TANZANIA BARA (TIC).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...