Na Khadija Seif Michuzi Tv
SHULE ya Scolastica inawakaribisha wazazi na walezi katika Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba Dar es salaam kupata ushauri wa Kiel na jinsi ya kujiunga na shule hiyo.
Akizungumza na Michuzi Tv Meneja Masoko wa Shule ya Scholastica inayopatikana katika Mkoa wa Kilimanjaro nje kidogo ya Mji wa Moshi amesema katika Maonyesho hayo mbali na kutoa Elimu jinsi ya kujiunga na shule Wazazi,walezi watapatiwa Elimu jinsi ya Kumuandaa Mwanafunzi kusoma Shule yenye ufaulu na inayofanya vizuri Kimkoa na Kiwilaya na inashika nafasi ya kwanza Kimkoa na ya 10 kitaifa.
"Nawakaribisha Sana Wazazi pamoja na wanafunzi kutembelea Banda letu katika Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba Dar es salaam ambapo tunatoa ushauri namna gani wataweza kujiunga na Shule ya Scholastica inayopatika katika Mkoa wa Kilimanjaro yenye ufaulu na inayofanya vizuri Kimkoa."
Hata hivyo ameeleza kwa namna gani itamnufaisha Mwanafunzi atakaehitaji kujiunga shule hiyo kufanya Majaribio awapo bandani hapo na baada ya siku kadhaa atapatiwa majibu yake .
"Upitapo Bandani utaweza kupatiwa Elimu na ushauri jinsi ya kujiunga shule hiyo pia Mwanafunzi atapatiwa fursa ya kufanya Majaribio ya kimazoezi (Interview) papo kwa hapo."
Pia Msuya amewatoa hofu Wazazi na walezi kuhusu Maadili ya shule hiyo na kuwaasa kuichagua shule hiyo kwa Elimu Bora zaidi na Malezi kwa watoto wao.
"Shule ni ya bweni kwa kidato Cha kwanza Hadi Cha sita na ya kutwa kwa Wanafunzi wa Msingi na chekechea ikijumuisha jinsi zote wakike kwa wakiume hivyo kwa namna moja au nyingine utaona jinsi gani swala la Maadili linazingatiwa ipasavyo Japo tabia kila mtoto ana makuzi yake lakini uwapo Shuleni watoto wote ni sawa wanafata vile shule ilivyoweka sheria zake".
Mwanafunzi akipatiwa ushauri namna ya kujiunga na Shule ya scholastica iliyopo Mkoa wa Kilimanjaro ambapo shule hiyo inatoa huduma ya Ushauri pamoja na interview ya papo kwa papo bandani katika Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba Dar es salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...