Charles James, Michuzi TV

CHAMA Cha Mapinduzi kimesema hakitahasimiana na Vyama vingine vya Upinzani kwani uwepo wao na neema na tija kwa chama Tawala katika kubaini kasoro na kuzipatia ufumbuzi kwa lengo la kuwatumikia Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka wakati wa kufunga kampeni za Ubunge Jimbo la Konde Pombe.

Uchaguzi wa Konde Pemba unafanyika Julai 18 mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekua Mbunge wake Khatibu Haji ambapo CCM yenyewe imemsimamisha Sheha Faki Mpemba kuwa Mgombea wake.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza Kwenye mkutano huo, Shaka amesema ni jambo la uongo kusikia wapo baadhi ya viongozi wanaosema CCM inakandamiza upinzani huku akisema CCM inaheshimu Demokrasia na kutambua umuhimu wa vyama hivyo.

" Ni jambo la uongo kuona watu wanasema sisi Chama Tawala tunakandamiza vyama vingine, tunafahamu umuhimu wa vyama vya upinzani katika kuleta maendeleo ya Nchi, Chama chetu chini ya Mwenyekiti na Rais Samia Suluhu Hassan tutaendelea kulinda demokrasia nchini.

Tutaendelea kuwaheshimu kwa sababu wote tunajenga nyumba Moja, CCM inafarijika kuona wapinzani wetu wanapotupinga kwa hoja kwani tunalizingatia hilo na tunajisahihisha," Amesema Shaka.

Amewataka wananchi wa Konde kumchagua Mgombea wa CCM, Shekha Mpemba Fakhi ili akaungane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi katika kuitekeleza ilani ya CCM ya kuwatumikia wananchi wote wa Tanzania.

" Zanzibar ya sasa haihitaji viongozi wepesiwepesi, na hapa kwenu Konde tunahitaji mtu shupavu, jasiri ambaye anaweza kuwavusha wananchi wake, mtu ambaye anaweza kusimama kuwatetea wanyonge wa hapa, msihangaike na wagombea wa upinzani ambao wamekua wanabeba ajenda zao na siyo ajenda za wananchi, " Amesema Shaka.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka akiongea na wananchi wa Jimbo la Konde Pemba ambao wamejitokeza katika kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo hilo, Shekha Fakhi Mpemba.
Wananchi mbalimbali ambao wamejitokeza katika kampeni za Ubunge wa Jimbo la Konde kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Shekha Fakhi Mpemba.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...