Tasisi ya kifedha ya kukopa na kuwakwamua wajasiliamali na wafanyabiashara nchini ,MMJ Microfinance imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa sherehe ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo na Uzinduzi rasmi,Mkurugenzi wa tasisi Bi. Esther Ogutu alisema ni furaha ilioje kufanikisha ndoto zake za kumiliki na kuongoza taasisi hiyo kwani ni changamoto nyingi wanapitia wanawake katika kusimamia taasisi za kifedha nchini.
kwani kufanya hivyo kunaongeza mtaji na kufanikisha malengo kwa wakati ,pia aliwaambia kuwa wafanyabiashara wakubwa duniani mikopo ya taasisi za fedha ndio imefanikisha malengo yao hivyo kutoogopa kukopa.
Mkurugenzi wa Tasisi ya kifedha ya MMJ Microfinance, Esther Ogutu (wa pili kushoto) na Meneja biashara wa CRDB tawi la TPA,Anande Mwasha (katikati) wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo ya mikopo uliofanyika jijini Dar es Salam.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...