*Nia kutaka fedha ya serikali isipotee pamoja na kunufaisha walengwa


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) imesema kuwa inatoa elimu kwa makundi wanaopata mikopo asilimia 10 katika Halmashauri ili kuwa na nidhamu ya fedha hizo na kuweza kuzirudisha.

Hayo yamesemwa na Mhadhiri wa Taasisi hiyo Mashaka Mbugi wakati alipokuwa akizungumza na Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zung aliyetembelea Banda la TIA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.Mashaka amesema katika kampasi zote wa Taasisi hiyo wameanza kutoa mafunzo ili kuhakikisha wanaopata mikopo ya serikali wanarudisha na kuendelea kutoa huduma zingine.

Amesema fedha wananchi wakipata wanakuwa na mambo mengi cha msingi ni kupewa elimu namna ya kuzitumia na kufikia malengo yao ya kukua kiuchumi.

Mashaka amesema kuwa fedha hiyo wanaweza kutumia kwa kuangalia faida ya kwa kutenga kwa asilimia kodi,kutoa sadaka msikitini au kanisani masuala mengine katika jamii hapo ndipo faida ya fedha hiyo itaonekana.

Aidha amesema kuwa katika Taasisi hiyo wamekuwa wakitoa masuala ya ushauri kwa wakaguzi na wahasibu ili kwenda kitaalam katika kufanya kazi zao.

Amesema kuwa katika maonesho hayo wanawezesha kufanya udahili kwa njia ya mtandao kwa kozi mbalimbali.

Hata hivyo katika kwenda na changamoto zinazowakabili vijana juu ya tatizo la ajira wanafundisha ujasiriamali na matokeo yameonekana kwa baadhi ya vijana waliohitimu wameweza kujiajiri na kuajiri vijana wenzao.
Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu akipata maelezo kutoka kwa  Mhadhiri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Mashaka Mbugi wakati alipotembelea banda la TIA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Caroline Mulungu  akizungumza na Wateja waliotembealea banda la TIA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu akipokea mchapisho mbalimbali zenye taarifa za Taasisi ya Uhasibu Tanzania wakati alipotembelea banda la TIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...