Waziri wa Awamu ya Tano na Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Sarah Goroi wakati alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.
Waziri awamu ya Tano  ya Tano na Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu akizungumza na waandishi Habari Katika Banda la Chuo cha Uhasibu Arusha( IAA) wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Awamu ya Tano ambaye ni Mbunge  Ilala Mussa Azzan Zungu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) alitembelea maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

*Amesema ni Chuo pekee kilichoona tatizo la vijana kukosa ajira.


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Waziri wa Awamu ya Tano na Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu amesema Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) wamejipanga katika kutoa elimu bora kwa vijana kwa kuanzisha program wezeshi za shahada ya kwanza zinazojulikana Kama “apprenticeship programmes” ambapo baada ya mwaka mmoja wanakwenda katika sehemu ya Mafunzo  ya kazi katika fani zao hivyo, chuoni anakaa muda mchache katika miaka Yake mitatu. 

Mbunge huyo ameyasema hayo katika Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam (Sabasaba)  alipotembelea banda la Chuo hicho , amesema kuanzisha program hizo  litatatua tatizo la vijana kutokuwa na uzoefu katika fani mara wanapomaliza. 

Amesema kuwa licha ya kufanya vizuri lakini wamejipanga ikiwa ni pamoja na Mafunzo kwa wahadhiri kwendana na mahitaji ya sasa katika utoaji wa elimu.

Aidha amesema kuwa Chuo hicho kinaonyesha uzalendo kutokana na kutambua changamoto katika jamii na kuja na suluhuhisho ya utoaji wa elimu katika kozi ambazo bado hazipo nchini.

"Chuo hiki wamekuwa wazalendo wa kweli katika kuanzisha program ambazo zinawakomboa vijana kuwa na fursa ya kuajiriwa na kujiajiri” amesema Zungu.

Amesema kuwa mwaka jana alipita katika maonesho ya Vyuo Vikuu na kutoa pongezi lakini wamejiongeza zaidi ikiwa ni Pamoja na kuanza kufundisha Cyber Security, Mobile Application na nyingine. 

Nae Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo hicho Sarah Goroi amesema kuwa ndani ya mwaka huu kinatarajia kuanzisha programu mpya ambazo Kati ya hizo ni za Shahada ya kwanza na Shahada ya Uzamili. 

Amesema kozi hizo zinazotolewa na Chuo hicho  ni kwa vitendo zaidi na sio kwa nadharia kwa lengo la kumwandaa mwanafunzi kujitegemea zaidi katika kujipatia ujuzi.

"Tunaisaidia Serikali kufikisha  malengo ya vijana kujiajili wenyewe zaidi kuliko kusubiri ajira tumejipanga  vizuri Kama Chuo” alisema  Goroi

Amesema  kwa mwaka huu wanatarajia kudahili  takribani Wanafunzi wapatao 10,000 katika kampasi ya Arusha,Dar es Salaam na Babati mkoani  Manyara.

Aidha amewakaribisha Wananchi kutembelea maonesho na judoka katika banda lao lililopi katika Jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...