Mkurugenzi
katika Kurugenzi ya Shahada za Juu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma,
Profesa Frowin Paul Nyoni akitolea ufafanuzi kwa wananchi waliofika
kwenye Banda la Udom kuhusu namna ya udahili kwa wanafunzi wapya wa
mwaka wa masomo wa 2021/22 kwenye Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya
Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Mhadhiri
msaidizi Idara ya Sanaa Bunifu na Taaluma za habari kutoka Chuo kikuu
cha Dodoma, Peter Msuya akitoa ufafanuzi kuhusu ubunifu wa sanaa za
mikono zilizofanywa na wanafunzi wa UDOM kwa maofisa wa Shirika la
Viwango Tanzania(TBS) waliotembelea Banda la chuo hicho katika Maonesho
ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri
Msaidizi Idara ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Miraji Hossein
akitolea ufafanuzi kuhusu mtambo wa kusafishia maji uliotengenezwa na
chuo hicho kwenye Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika
katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri
Mwandamizi ambaye ni Mratibu katika kurugenzi ya Shahada za Juu kutoka
UDOM, Dkt. Peter Josephat Kirigiti akisikiliza maswali kutoka kwa
mwananchi aliyegifika kwenye Banda la chuo hicho alipokuwa anataka kujua
namna gani wanafunzi wanavyoweza kufanya udahili kwa njia ya mtandao
katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri
kutoka Idara ya Uhandisi wa Mawasiliano, Mkuuwa Idara ya Ubunifu na
Ujasiriamali chuo kikuu cha Dodoma, Dkt. Alex Frank Mongi akitoa maelezo
kuhusu ubunifu wa teknolojia unaofanywa na Chuo hicho kwa maafisa wa
TBS waliotembelea Banda la chuo hicho.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...