Na Marco Maduhu, Shinyanga.
UMOJA wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Shinyanga, ume muunga mkono Rais Samia Suluhu Hassani, kuwa hawakubaliani na wazo la kuanzishwa kwa mchakato wa katiba mpya.
Amesema chama hicho hakina ajenda, wala wazo la kuanzisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya, bali wana kazi kubwa ya kujenga nchi na kuwaletea maendeleo wananchi.
"Jana kuna chama flani kilikaa kikao na kumtaka Rais Samia aanzishe mchakato wa katiba mpya , hiyo siyo ajenda ya CCM, bali kwa sasa tuna kazi ya kujenga nchi"amesema Shemahonge.
"Tuna muunga mkono Rais wetu Samia kwa kukataa Jambo hilo la mchakato wa katiba mpya, ambapo kwa sasa nchi ipo kwenye vita ya kuinuka kiuchumi, kwa kupambana na na janga la Corona na siyo katiba mpya," ameongeza.
Pia amewaka vijana, na wanachama wa CCM, kutembea kifua mbele pamoja na kumuunga Mkono Rais Samia, kutokana na kazi kubwa ambayo ameifanya kwa watanzania ndani ya kipindi chake cha siku 100.
Aidha Baraka amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kuwajali vijana kwa kuwaamini kwenye Serikali yake na kuwapatia ajira, huku akiendelea kuzalisha ajira nyingine kupitia ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwamo Reli ya kisasa na Bomba la mafuta.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Agnes Bashemu, amewataka vijana wa chama hicho, kuachana na Makundi, bali washikamane kukijenga chama.
Tazama picha hapa chini
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge Kushoto, akizundua Shina la wakeleletwa la vijana tawi la Negezi Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga, kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, akifungua Ofisi ya CCM tawi la Negezi Kata ya Mwawaza.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, akizungumza kwenye uzinduzi wa Shina la wakeleketwa la vijana wa CCM tawi la Negezi Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Muhsin Zikatim, akizungumza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa Shina na Ofisi ya CCM tawi la Negezi Kata ya Mwawaza.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Agnes Bashemu, akizungumza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa Shina na Ofisi ya CCM tawi la Negezi Kata ya Mwawaza.
Viongozi wa CCM na UVCCM wakipiga picha ya pamoja, mara baada ya kumaliza kuzindua Shina na ufunguzi wa Ofisi Tawi la Negezi Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...