Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mika na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akikagua vifaa tiba vilivyotolewa na Benki ya Maendeleo TIB kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia afya) Dkt. Grace Magembe na kushoto ni Meneja Masoko na Uhusiano wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Saidi Mkabakuli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mika na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akimsikiliza Meneja Masoko na Uhusiano wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Saidi Mkabakuli (kushoto) wakati wa makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia afya) Dkt. Grace Magembe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mika na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipata ufafanuzi wa matumizi wa moja ya mashine zilizotolewa na Benki ya Maendeleo TIB kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma kutoka Meneja Masoko na Uhusiano wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Saidi Mkabakuli (katikati). Wanaosikilizia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye (kushoto) na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Robert Rwebangira (nyuma).


Na Mwandishi wetu Kasulu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wadau wa maendeleo nchini kuwekeza katika rasilimali watu ili kupata watumishi wenye weledi katika kutoa huduma bora ya afya kwa jamii.

Waziri Ummy ametoa wito huo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma mara baada ya kupokea vifaa tiba katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu vilivyotolewa na Benki ya Maendeleo TIB kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Alisisitiza kuwa kwa sasa kipaumbele cha Serikali ni miradi inayogusa maisha ya wananchi hasa katika seka za afya, miundombunu, elimu na maji katika ngazi ya msingi.

“Tunawasihi wadau wote wa maendeleo nchini kuelekeza nguvu zao katika kuwekeza kwenye miradi inayowalenga moja kwa moja wananchi badala ya kutenga bajeti kubwa kwa ajili mafunzo na semina,” alisema Ummy.

Waziri Ummy aliongeza kuwa wadau wengi wa afya wamekuwa wakiwekeza sana katika semina na mikutano na kusahau kuwa vifaa vinavyoletwa kwa ajili ya kutolea huduma vinahitaji kuwa na wataalam ambao wanauwezo wa kuvitumia.

Aliwataka viongozi wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanapokaa na wadau wa maendeleo wahakikishe wanatoa vipaombele vitakavyosaidia kuleta mabadiliko katika sekta ya afya na elimu nchini.

Waziri Ummy ameishukuru Benki ya Maendeleo TIB kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha huduma za afya ya msingi kwa kutoa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 12.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Meneja Masoko na Uhusiano wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Saidi Mkabakuli alisema kuwa benki imetoa msaada huo kwa kutambua ukweli kuwa sekta ya afya ni mojawapo ya eneo la kipaumbele katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo.

“Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta ya afya nchini TIB kama benki inayotekeleza vipaumbele vya serikali, tuliona ni vyema kuchangia baadhi ya vifaa tiba kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kasulu kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali za kuimarisha Huduma za Afya ya Msingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini,” alisema.

Aliongeza kuwa msaada huo unalenga kusaidia mpango mkakati wa OR-TAMISEMI ambao unatekeleza malengo mahsusi kama vile kuimarisha na kuhakikisha vituo vya kutolea huduma vilivyokamilika vinaanza kutoa huduma za Afya ikiwa ni pamoja na ununuzi wa dawa, vitendanishi, vifaa na vifaa tiba.

Bw. Mkabakuli alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa taasisi nyingine za kifedha kuchangia jitihada za Serikali za kuboresha sekta ya afya nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...