Dodoma- Julai 22, 2021 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Mhe, Innocent Lugha Bashungwa (Mb)  amewateua Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Taifa CUP, kwa ajili ya  kusimamia mashindano ya mwaka 2021. 

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hassan Abbasi imefafanua kuwa, kamati  hiyo inaongozwa na Mwenyekiti, Yusuph Singo Omary ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya  Maendeleo ya Michezo nchini na Makamu wake, Ameir Mohammed Makame ambaye ni  Kamishna wa Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wajumbe wengine 12. 

Wajumbe 12 wa Kamati hiyo ni kama wanavyoonekana hapa chini: 

  1. Bw. Shaibu Muhamed. Kamishna wa Vijana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 2. Bi. Neema Msitha. Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa 3. Bw. Jackson Ndaweka. Katibu Mkuu Shirikisho la Riadha Tanzania 4. Bw. Michael Mwita. Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania 5. Bw. John Nguchiru. Katibu Mkuu Chama cha Michezo ya Jadi 6. Bw. Wilfred Kidao. Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania 7. Bw. Leonard Thadeo. Mratibu wa Michezo, OR-TAMISEMI 8. Bw. Shaffih Dauda. Mdau wa Michezo 
  2. Bw. Mbaki Mutahaba. Mdau wa Michezo 
  3. Bw. Ally Mayai. Mdau wa Michezo 
  4. Bi. Eunice Chiume. Mwakilishi wa Benki ya NMB 
  5. Bw. William Kallaghe. Mwakilishi wa Benki ya NBC 

Aidha, Waziri Bashungwa amesema mashindano hayo yatafanyika mwezi Desemba mwaka  huu na yatahusisha baadhi ya michezo ya kipaumbele. Michezo ya kipaumbele inajumuisha Soka, Riadha, Ngumi, Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu na Mpira wa Pete (Netiboli).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...